Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KOCHA mkuu wa zamani wa AS Vita Club ya Kinshasa, Jean Florent Ibenge Ikwange, amekamilisha dili lake huko Morocco, baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili kujiunga na RS Berkane.
Ibenge, mwenye umri wa miaka 59 ambaye hivi karibuni alimaliza muda wake wa miaka tisa huko Vita Club na sasa amesaini mkataba mnono wenye thamani ya dola 55,000 kwa kila mwezi ambapo miaka miwili atajinyakulia Mil.127 ya Kitanzania.
Kocha huyo,alijiunga na Vita Club mnamo Februari 2012 kutoka klabu ya China, Shanghai Shenshua FC na baadaye aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa Timu ya taifa ya Congo miaka miwili baadaye.
Hata hivyo, Ibenge ndiye Mshindi wa taji la ligi huko DRC Mwaka 2014 na 2018 pamoja na mshindi wa pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2014 na Kombe la Shirikisho 2018.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania