November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Huyu Daktari wa wagonjwa wa Corona kaamua kujinyonga

Alikuwa mstari wa mbele vita ya corona, Inadaiwa wauguzi wengi wanapitia wakati mgumu

VIRGINIA, Daktari Mkuu katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Manhattan nchini Marekani ambaye aliwatibu wagonjwa wengi wa virusi vya corona (COVID-19), Dkt.Lorna M. Breen amejiua kwa kujinyonga.

Kwa mujibu wa The New York Times, baba yake mzazi na Jeshi la Polisi mjini Charlottesville, Virginia wamethibithisha kifo hicho.

Dkt.Breen ambaye pia alikuwa ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Dharura katika Hospitali ya NewYork-Presbyterian Allen alijinyongea mjini Charlottesville, Virginia ambapo alikuwa anaishi na wazazi wake.

Dr. Lorna M. Breen ambaye aliamua kujiua, picha kubwa ni hospitali aliyokuwa anafanya kazi

Msemaji wa Jeshi la Polisi mjini Charlottesville,Tyler Hawn ameeleza kupitia barua pepe kuwa, maafisa wa jeshi hilo siku ya Jumapili iliyopita walipokea simu ya dharura ikihitaji msaada wa kitabibu.

“Mgonjwa (Dkt.Lorna) alichukuliwa na kupelekwa Hospitali UVA kwa matibabu, lakini baadae aliamua kujijeruhi mwenyewe,”amesema Hawn.

Baba yake Dkt.Lorna Breen, Dkt.Philip C. Breen amesema, baada ya binti yake kubaini hali yake si njema aliamua kufanya uamuzi ambao si wa busara.

“Alijaribu kufanya kazi yake kwa kadri ya uwezo wake na ikamuua,”amesema Baba mzazi wa marehemu huyo.

Dkt.Philip Breen amesema, binti yake awali alikuwa ameambukizwa virusi vya corona, lakini alikuwa amerejea kazini baada ya kupona wiki moja na nusu iliyopita.

HABARI KAMILI IKO GAZETI LA MAJIRA TOLEO LA ALHAMISI…