December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Husein foundation yawakumbuka wahitaji

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

TAASISI ya Hussein Husein Foundation yatoa msaada wa vyakula kwa makundi maalum katika kituo cha Watoto Yatima cha Ahsante Community Tanzania, kilichopo Bombambili wilayani Ilala mkoani Dar-es-Salaam.

Msaada huo ulitolewa na uongozi wa taasisi hiyo ukiongozwa na Mkurugenzi Husein Husein ambaye ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.

Ameeleza kuwa wamekuwa karibu na serikali katika kusaidia jamii na makundi maalum kwa kutoa mahitaji mbalimbali.

“Leo ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa,kupitia taasisi yetu tumefanya ziara Hospitali ya Wilaya Kivule kuonana na wajawazito, waliojifungua leo na kuwapa pole na mahitaji ikiwemo sabuni za kufulia kisha tumeshiriki chakula cha mchana na watoto wa makundi maalum na kuwapa misaada ya chakula pamoja na vyandarua,”amesema Husein.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule Amos Hangaya, ameishukuru taasisi hiyo kusaidia jamii kwani kila mwaka imekuwa sehemu ya utaratibu wake wa kula chakula na watoto wa makundi maalum pamoja na kutoa msaada wa vyakula mbalimbali.

Amos amewataka watoto wa Kituo cha Asante Community Tanzania wazingatie masomo ili waje kuwa viongozi wa baadae wasijipe unyonge kwani taifa lolote ili liweze kuendelea linaitaji watu wake waweze kusoma.

hivyo atuna budi kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya elimu imejenga shule nyingi za msingi na sekondari.

Aidha Amos amesema watu wanaohitaji kutoa sadaka wafanye ziara katika vituo vya watoto wa makundi maalum na kuisaidia jamii hiyo ili nao waweze kujisikia furaha .

Msimamizi na Mlezi wa Kituo cha Asante Community Tanzania Nurudini Ulaya, amesema changamoto inayowakabili kituoni hapo ni eneo dogo,uchakavu wa jengo inayosababisha mpaka leo Serikali bado aijawapa usajili.

Nurudini Ulaya amesema kituo hicho kilianza 2018 kikiwa na watoto 12 kati yao wasichana 7 na wavulana watano kwa sasa kituo kina watoto 23 wavulana 13 na wasichana 10 wanasoma shule ya msingi na shule ya awali