Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
HAKIMU Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Yusto Ruboroga ameahirisha hukumu ya kesi ya madai namba 53/2017 iliyofunguliwa na wahasisis na wanachama wa taasis ya Fiysabillillah Tabligh Markaz dhidi ya kiongozi Mkuu wa Taasisi hiyo Hadi Desemba 21 mwaka huu Ili ajipe nafasi zaidi ya kuimalizia hukumu hiyo
Mdaiwa katika kesi hiyo ni Abdallah Abubakar ambaye ni kiongozi mkuu wa Taasisis ya Fisabilillah Tabligh Markaz iliyopo Gongolamboto jijini, Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Abdumalik Khof na Al Amin Rajab Juma ambao ni waasisi na wanachama walnamlalamikia mdaiwa Abdala Abubakar kwa ubadhirifu wa mali za taasisi hiyo na uongozi mbovu dhidi ya kiongozi huyo.
Wanadai kuwa kiongozi huyo amekuwa akiuza mali za taasisi bila kufuata utaratibu na kutumia fedha kwa maslahi yake
Madai Yao ni kwamba mdaiwa amekuwa akiuza viwanja , magari, na vitu mbalimbali ambaxo ni mali za taasisi kiholela
Pia amekuwa akiwafukuza uwanachama bila kufuata utaratibu wa katiba ya taasisi hiyo.
Pia wanachama hao wanamlalamikia kiongozi huyo kwa uongozi mbovu ikiwemo kufukuza wanachama waanzilishi kwa maslahi yake bila kufuata utaratibu
kiongozi huyo alikuwa madarakani tangu mwaka 1996.
Kutokana hali hiyo, wanachama hao wanaiomba mahakama kumuondoa madarakani kiongozi huyo ili kuepusha uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza.
Pia wanaiomba mahakama kutoa amri ya kufanyika kwa ukaguzi wa hesabu na mali zote za taasisi hiyo na watakaobainika kufanya ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.
Pia wanaiomba mahakama itoe amri ya kuwarejesha wanachama waliofukuzwa bila utaratibu.
More Stories
Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauaji wakigombania shamba
Ng’ombe 10 wamekufa kwa kupigwa na radi
Rukwa waanzisha utalii wa nyuki