January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),Sabanitho Mtega akiongea na waandishi wa habari Jana jijini Da es Salaam katika viwanja vya maonesho ya sabasaba.

Huduma za GCLA zaboreshwa

Na Penina Malundo,timesmajira,Online
MKURUGENZI  wa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),
Sabanitho Mtega amesema Mamlaka hiyo   kwa sasa imejipanga kikamilifu katika kutoa huduma kwa wananchi kutokana na kuwepo kwa  wataalamu wa kutosha na mitambo mbalimbali ya uchunguzi.

Akizungumza hayo leo  Mkurugenzi huyo,Mtega wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja wa maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa maarufu sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Amesema kutokana na kujipanga huko kunarahisisha  utoaji wa majibu kwa haraka zaidi baada ya kufanya uchunguzi wa sampuli mbali mbali.
“Kwa mwaka huu Serikali imetupatia wataalamu wa kutosha ambayo kila kukicha wamekuwa wakipata ujuzi unaowawezesha kufanya kazi kwa weledi na kujitegemea,” amesema na kuongeza 
” Pia mitambo katika eneo la huduma za kiuchunguzi tumekuwa tukifanya uchunguzi wa sampuli mbalimbali kama vile dawa asili, vyakula, kemikali, viwatilifu pamoja na sampuli za mazingira na kuongeza kuwa baada ya kufanya uchunguzi huo utoa majibu kwa ajili ya kusaidia mamlaka za udhibiti kufanya maamuzi stahiki,”amesema
Mtega amesema  majukumu ya mamlaka hiyo yametengwa katika maeneo matatu, ambapo eneo la kwanza ni huduma za kiuchunguzi wa sampuli mbalimbali, huduma za kisheria na utoaji wa ushahidi mahakamani.
Amesema pia wamekuwa wakifanya uchunguzi wa sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai kama vile dawa za kulevya, ambapo baada ya kuchunguza uwasilisha matokeo kwenye mamlaka husika kwa ajili ya maamuzi ya kisheria.
“Pia sisi ni mamlaka ya udhibiti unaosimamia kemikali za majumbani na viwandani hivyo katika hali hiyo kemikali zote zinazoingia nchini lazima sisi kama mamlaka tuwasajili wale wote wanaoziingiza na kutoa kibali kwa ajili ya kusafirisha ndani na nje ya nchi kemikali hizo,” amesema 
Amesema kwa hali hiyo wamekuwa wakifanya ukaguzi kwa saa 24 kila siku na kuomgeza kuwa wana wakaguzi wao katika kila mipaka nchini kwa ajili ya kuharakisha utoaji wa mizigo na kuangalia kemikali zote zinazoingia nchini zina ubora unaokubalika na zinatumika kwa malengo yaliyoletewa na si vinginevyo.