February 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Huduma ya kusafisha figo yasogezwa Manyara

Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Bahati

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga,amesema kwa mara ya kwanza Mkoa huo utaanza kutoa huduma ya kusafisha Figo(dialysis).

Sendiga ameyasema hayo Februari 6, 2025 wakati akizindua rasmi Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara,ambapo ameeleza kuwa huduma ya usafishaji wa figo itatolewa ndani ya siku 5-6 kuanzia Februari 6, 2025, na hivyo kuwata wananchi kutumia siku hizo kwa ajili kupata huduma hiyo.

Ambapo Mkoa wa Manyara,umepata mashine 6 za usafishaji wa figo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo, zitakua na uwezo wa kusafisha damu za wagonjwa 12 kwa siku, ambapo zitasaidia kupunguza adha, gharama na muda kwa wagonjwa ambao wamekua wakifuata huduma hiyo mbali ukilingamisha na Sasa itakua ikipatikana ndani ya Mkoa husika.

Sendiga ameiwaasa bodi hiyo akiwemo Mwenyekiti na wajumbe,kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa uadilifu, uwazi na kwa kuzingatia maslahi ya jamii
na si vinginevyo

Aidha amesema kazi kubwa ya bodi hiyo ni kushauri uongozi wa hospitali, kusimamia huduma bora kwa wananchi pamoja na matumizi sahahi ya rasilimali zilizopo hospitalini hapo.