Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano Askofu Dkt.Evance Chande amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na hotuba aliyoitoa jana kwenye uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dodoma ,Dkt.Chande amesema hotuba imesheheni matumaini lukuki kwa watanzania na hivyo kuifanya jamii kuendelea kuwa na imani naye.
“Kwa hotuba aliyoitoa Rais Samia jana ,kwa mtanzania mwenye nia njema na nchi yake lazima amkubali,ingawa yeye anasema amevaa viatu vya hayati Rais John Magufuli na ni vikubwa kwake,lakini mimi nasema viatu hivi vimemtosha..,na ninaweza kusema amemzidi Dkt.Magufuli hasa kwenye Mahusiano ya Kimataifa maana ameaminika na kupewa fedha hizo.”amesema Dkt.Chande na kuongeza kuwa
“Nimemsikiliza kwa makini na kubaini kuwa katika kipindi cha miezi sita ya utawala wake amelibadilisha Taifa katika masuala ya kimataifa na kufanikisha kulishawishi Shirika la Fedha Duniani (IMF)kuipatia nchi fedha nyingi kiasi cha sh.Trilioni moja,kiasi hiki ni kikubwa hasa kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na janga la Corona”amesema kiongozi huyo
Vile vile amempongeza Rais Samia kwa namna alivyotoa maelekezo ya fedha hizo kwenye matumizi yatakayokwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali inayokwenda kutekelezwa kupitia fedha hizo.
Kiongozi huyo amesema,Rais Samia amedhamiria kuliondoa Taifa kwenye ,maambukizi dhidi ya virus vya CORONA kutokana na kuleta chanjo nchini ili wananchi waweze kuchanja na kujiondoa kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.
“Nimeona kwenye fedha hizo zinakwenda kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ununuzi wa magari ya kubebea wagonjwa ,miundombinu ya maji,afya,elimu na mingine mingi,hii ni dhamira nzuri na yenye nia njema kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.”
More Stories
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM