Na Penina Malundo
MAZINGIRA wanayoishi baadhi ya wanafunzi wa kike wa Vyuo Vikuu nchini yanatia hofu ya uwezekano wa ongezeka la vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokana na namna wanavyoishi.
Ukatili wa kijinsia ni miongoni mwa changamoto ambazo watu wanakumbana nazo ikiwemo kunyanyaswa,kupigwa,kutelekezwa na hata wanaofanyiwa ngono bila ridhaa zao wengine wakiwa na umri mdogo.
Ni dhahiri shahiri kuwa baadhi ya wanafunzi wa kike wanayoishi nje ya mazingira ya vyuo wamekuwa wakijihusisha na biashara ya ngono kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukata.
Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, gazeti hili lilipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kudai kuwa wanafunzi wengi wanajiingiza katika biashara ya ngono kwa sababu mbalimbali ikiwemo uchache wa hosteli, tamaa za maisha na kufuata makundi mabaya ya marafiki.
Amina Jumaa (sio jina halisi) anasema ukatili mkubwa wanaolia nao katika vyuo ni pamoja na uchache wa hosteli kwa watoto wa kike, hali inayofanya kufunga ndoa za mikataba za miaka miwili na wengine kuishia kujihusisha na biashara za kuuza miili ili kuweza kupata fedha za kujikimu Ili wapate fedha za kulipia hosteli za nje,
Anasema wanafunzi wakike wamekuwa wanapitia wakati mgumu sana katika kupata sehemu za kulala wanapotoka hosteli za chuo wakiwa mwaka wa kwanza.
“Sisi tunalia na uchache wa hosteli (vyumba vya kulala) wanafunzi kuanzia mwaka wa pili hadi watatu vimekuwa mwiba mkali kwetu watoto wa kike wa Chuo kumudu maisha inakuwa ni changamoto,anasema na kuongeza:
“Dada unajikuta unajiingiza katika ndoa za mikataba ambapo mwanafunzi akimaliza chuo kila mtu anakwenda kivyake,”anasema na kusisitiza ndoa hizo zinahusisha aidha wanafunzi kwa wanafunzi ama watu wa nje ambao hatufahamiani kabisa
Anasema wamekuwa wakilazimika kujiingiza kwenye biashara ya kuuza miili ili waweze kupata fedha za kujikimu kimaisha
Anaongeza kuwa kutokana na kipanda kwa gharana za maisha pia fedha za mikopo wanazopata kutoka serikali ni ndogo hazikithi mahitaji yote.
“Ni kweli kuwa wapo baadhi ya wanafunzi wanaojiuza kutokana na tabia zao, pia wapo wanaojiuza kwa kufuata mikumbo ya marafiki baada ya kukosa fedha za kulipia pango ,”anasema
“Dada nenda pale Riverside Ubungo asilimia kubwa ya wanafunzi wa kike wanaoishi pale ikifika majira ya jioni utawakuta barabarani wanajiuza na hii ni kutokana na kutokuwa na hosteli za kutosha vyuoni.
Anasema mazingira ya hosteli za nje ni mabaya sana kwani si rafiki na watoto wa kike
Anataja kiasi cha fedha wanachokipata wanafunzi hao kwenye biashara hiyo ya kuuza niili kuwa ni kati ya Sh.2,000 hadi Sh.3,000 kwa kila mwanaume wanayekutana naye hiyo ni huduma ya chapchap inayofanywa wazi si faragha (vyumbani).
‘’Hapo unakuta mtu boom limekata,unadaiwa kodi ya nyumba uliyopanga hivyo unajikuta unaingia tu kufanya biashara hii bila hofu yoyote ya kupata magonjwa au nini na ukiingia katika hii biashara kutoka kwake ni kugumu sana,”anasema na kuongea.
Na hii bei ya Sh. 2,000 Hadi 3,000 ni kwa wale wanaojiuza pale riverside,ila nimesikia siku hizi kuna wengine wanajipanga kule Hosteli za Magufuli kuanzia saa nne hivi usiku napo kumeanza kushamiri kwa biashara hiyo,”anasema na kuongeza.
“Tena wale wa hosteli za Magufuli baadhi yao wanaile spesho oda ambapo ikifika tu saa mbili au tatu hivi magari yanakuwa yanamiminika kuwafuata yaani wateja wanakuwa wanafanya booking kwa simu,”anasimulia huku akisikitika
Anasema mbali na hiyo pia kuna kujiuza kwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile ili apewe 500,000 kwa siku na hii unakuta anafanya tendo la ndoa la mwili wote(All sex) kwa ajili ya kupata fedha za kujikimu kimaisha.
Amina anasema inauma sana kuona mabinti wadogo wakijiingiza katika biashara hii na ukizingatia wengine wametoka huko mikoani hata mambo ya mjini hawayajui.
Anasema endapo serikali ikiweka mazingira mazuri ya uwepo wa hosteli nyingi itasaidia kwa kiasi chake kupunguza biashara hii.Â
” Hosteli zikiongezwa na wanafunzi wa kike wakapewa kipaumbele hali hii inaweza kupungua kwa kuwa tunakuwa katika mazingira mazuri ya chuo na uangalizi mzuri kwao,”anasema na kuongeza kuyaomba Mashirika Yasiyo ya Kiserikali au Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iangalie namna ya kuwasaidia wanafunzi hawa kwasababu wengi wao unakuta wanafikia hatua ya kushuka katika masomo yao na kushindwa kufikia GPA zinazotakuwa huku wengine wakifeli kabisa.
Pia anasema ni vema masomo yawe yanatolewa mara kwa mara ya kuonesha namna ya kuishi maisha ya kuishi chuoni kuanzia elimu za sekondari ili mwanafunzi anapoingia chuoni ajue anakutana na kitu gani.
”Mfano nilipokuwa mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuna kesi ilitokea ya kubakwa kwa mwanafunzi mmoja kule maeneo ya Msewe tena alibakwa na wanaume wawili ile kesi haikuweza kusuluhishwa na mpaka leo yule Dada amebaki anaumia na kovu moyoni,”anasema.
Anasema kesi kama hiyo inatokea ni kutokana na hosteli kuwa chache wasichana kupanga mitaani,huku wanaume wanakuwa wanawinda na endapo unataka kupelekeka kesi kama hii chuoni wanahitaji vielelezo wakati tayari mtu kaumia.
Naye mmoja wa kiongozi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam jina linahifadhiwa,anasema yeye ni kiongozi katika chuo hicho mambo mengi yanatokea kwa wanafunzi wanawake kutokana na changamoto ya malazi.”Unajua chuo chenyewe hakina nguvu ya kujenga hosteli au kuboresha majengo yake ila wanauwezo wa kushawishi serikali kuongeza hosteli kwaajili ya wanawake kwani tunakumbana na changamoto nyingi za ukatili,”anasema na kuongeza
“Hosteli zinapokosekana zinapelekea kujiingiza katika mahusiano ambayo sio sahihi na kujikuta tunatumikishwa wakati wa masomo wewe unajikuta unapika au unafua hata muda wa kwenda chuo kuingia katika kipindi unakosa,”anasema .
Anaeleza mwanafunzi anakuja kutoka mkoani hana ndugu Dar es Salaam nakaa mwaka mmoja hosteli za chuo mwaka wa pili anaambiwa atoke akajitafutie hostel za nje wakati mwingine anaboom lakini boom hilo ni dogo na halitoshi kukidhi mahitaji yake anaona bora akajiwekeze kwa mwanaume.
“Kilio chetu kikubwa sisi wasichana hapa UDSM tunahitaji hosteli,siku 16 hizi za ukatili wa kijinsia tunaendelea kuhamasisha Serikali iweze kutuongezea hosteli kwani ,mtu akikaa hostel anaweza kushinda vishawishi vingi kuliko ile mtu kwenda kujipangia mwenyewe,”anasema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt.Lulu Mahai anasema ni kweli kuna Changamoto ya hosteli katika chuo chao na ni miongoni mwa Changamoto kubwa wanayoipata Chuoni hapa ni kwenye malazi kwa wanafunzi wao.”Changamoto wanayopata watoto wakike katika Chuo hichi ni sawa na sehemu nyingi ya Vyuo ambapo kuna malazi upungufu,”anasema na kuongeza
“Mfano katika chuo chetu kikuu cha Dar es Salaam kuna upungufu wa malazi ambapo yanaweza kuwacommodate (kutosheleza)wanafunzi 10000 hadi 11000 na unakuta nafasi tunaitoa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza zaidi ambaye amekuja kwa mara ya kwanza Dar es Salaama na hana mahali pa kufikia kwahiyo nafasi hiyo ndo tunaowapatia,”anasema.Â
Anasema wanaamini nao wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakimaliza mwaka huo na kuingia mwaka wa pili tayari Dar es Salaam anakuwa kashaijua na nirahisi kwake kuanza kutafuta malazi ya nje ambayo ni binafsi zinakuwa chini ya ofisi ya mshauri wa wanafunzi ambapo wanafunzi wanaonyeshwa ni maeneo gani ni salama ya kwenda kuishi.
***Akizungumzia wanafunzi kupanga nje ya hosteli za chuo
Anasema watu wa nje wanaopangisha nyumba uwa wanaleta maombi yao chuo kama wananafasi za kupangisha kwa wanafunzi wa chuo chetu,kwa hiyo mwanafunzi akitaka kupanga chumba uwa anapita kwa mshauri wa wanafunzi(Dean of Student)na kuweza kupata maelekezo ya wapi anaweza kupata nyumba yenye mazingira mazuri kuliko yeye mwenyewe kujitafutia wapi akakae ambapo anakutana na changamoto.
“Unakuta hosteli zetu mfano za mabibo au Magufuli Hall 7,8 na 9 ni za wasichana ila tunatoa nafasi kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza zinazobaki sasa uwa zipo kwenye online system tunaachia kila mtu anayehitaji kufanya shopping na kulipa kwa madarasa ya juu mwaka wa pili na watatu,”anasema.Â
Anasema chuo chao kinamkakati mkubwa wakuongeza malazi(hostel) kwa wanafunzi kupitia mradi wa higher Education transformation E ambapo kuna jengo la wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao wahawawezi kukaa pekee yao na pia Chuo chao bado kinafanya ukarabati wa baadhi ya majengo yake ili kuweza kuingiza wanafunzi wengi zaidi.
“Mikakati kama mikakati miaka 10 ijayo hali itabadilika sana Chuo kikuu kinajipanga kwa kweli kupanua nafasi za wasichana mahali pa kulala, na wanampa nafasi mtoto wa kike kutokana na changamoto nyingi anakutana nazo hasa mtaani au akikaa nje ya chuo hata ile umakini wa masomo inakuwa ni ndogo kwani ni rahisi kudanganyika,rahisi kukutana na vikwazo,”anasema na kuongeza
” Kama huku tunanjia ya msewe,changanyikeni watu wanapita katikati ya pori ni risk kubwa lakini tumekuwa tukiwashauri wawe wanatembea kwa makundi,tunafanya semina na ushauri kwa hawa watoto ili kuishi wao kwa wao kujitambua na kujithamini ,”anasisizaÂ
***Wanafunzi wanaojihusisha na mahusiano
Anasema kama kweli kuna vijana wa chuo wanawake wanapanga nyumba moja na wanafunzi wakiume huko ni kujiozesha wenyewe bila mahali.”Kama ni kweli wanafunzi wetu wanalala hivyo na kujiingiza katika Mahusiano na wanafunzi wenzao au watu baki kisa malazi ambayo chuo hayajarasimishwa nadhani Mwandishi umetupa kitu cha kuwasaidia zaidi wanafunzi wetu kuwapa elimu ili waweze kujitambua katika nafasi zao ukiwemo kutojirahisisha kwa sababu ya Changamoto zao wanazopitia na sio kujiingiza katika matendo yasiofaa ya kuishi na wanaume wanapokuwa masomoni,”anasemaÂ
Anasema Chuo kikuu cha Dar es Salaam kimeanzisha dawati la kijinsia na kazi kubwa la dawati ni kupokea malalamiko kwa wanafunzi na wafanyakazi,sisi wanafunzi wakileta kesi cha kwanza ni kuichakata kesi na kuona ni aina gani ya ukatyioli uliofanyika kama wa kimwili,kisaikojia,au kingono au kiuchumi.
Naye Rais was Chuo Kikuu (DARUSO)… Mwandishi alipompigia simu juu kuhusu Changamoto ya wanafunzi wakike kujiingiza katika Biashara za kujiuza miili kutokana na ukosefu wa hosteli,anasema taarifa hizo hakuwa nazo hivyo ataanza kuzifanyia kazi na endapo akipata jibu ataweza kurudi kwa Mwandishi na kuzungumza nae.
“Kwa kweli sina taarifa kabisa kuhusu wanafunzi wetu kujihusisha na masuala ya Biashara ya ngono ,subiri nifatilie na nikishapata jibu nitaweza kukutafuta mwenyewe,”anasema
Aidha Naibu Waziri wa Elimu …Kupanga alipotafuta kuuliza suala hili la uhaba wa hosteli kuchangia kushamiri biashara ya ngono kwa wanafunzi wa Chuo kikuu na mkakati wa serikali katika kuongeza hosteli anasema swali hili linapaswa kuuliza wahusika sio Mimi (Mtafute Waziri anaweza kuzungumzia vizuri suala hili).
Mmoja wa Wakazi wanaoishi maeneo ya Riverside Ubungo,Athuman Said anasema ikifika majira ya saa 12 jioni hapa kituoni Mambo yanaanza watu wanavaa vibaya wanasimama barabarani hata kupita na watoto ni aibu kubwa sana.
“Hapa Riverside wanaojiuza miili wanachanganyika wapo watu wakawaida na wale wanafunzi wa Chuo ni aibu sana ikifika saa 12 jioni ndo wanaanza kuingia kazini Ila kuanzia kama saa mbili mbili hivi ndo panachanganya sasa na beii zao sio kubwa kuanzia 2000 hadi 10000 ukimzidishia labda umependa wewe,”anasema.
Anasema suala hili ni la kuangalia kwa umakini na kutilia mkazo serikali iangalie makundi haya yanateketea na ndo maana takwimu za Ukimwi zipo kwa watoto wadogo Kati ya miaka 18 hadi 24 no kutokana na Mambo kama haya.” Serikali ingechukua hatua za haraka kutusaidia kuongeza hosteli vyuoni,kuweka ulinzi mzuri na kutoa elimu kwa wanafunzi za Mara kwa Mara ili kusaidia kundi la wanafunzi kuwa salama zaidi,”anasema
Mmoja wa Madereva Bajaji wa Kituo Cha Riverside,Hassan Ali(sio jinalake halisi) anasema ni kawaida kwa baadhi ya watu kutumia Bajaji zao kama chumba kwa kukodi kwa muda mfupi kwaajili ya kushiriki tendo la ndoa.
“Sisi tunakesha hapa stendi tukisubiri abiria ikishafika mida ya saa mbili,dada zetu wanakua tayari wapo nje tunaita “sokoni”wakianza kujinadi,hivyo wanapoahindwana Bei ya kwenda nyumba ya wageni wanakuja kukodi Bajaji zetu kwa muda mfupi tunaweza kuwachaji kuanzia 5000,”anasema .
More Stories
Ubunifu wa Rais Samia kupitia Royal Tour unavyozindi kunufaisha Tanzania
Rais Samia anavyojenga taasisi imara za haki jinai kukabilina na rushwa nchini
Rais Dk. Samia alivyowezesha Tanzania kuwa kinara usambazaji umeme Afrika