Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
HOSPITALI ya Wilaya Wete Kinyasini, imekabidhiwa vifaa tiba mbali mbali na Kampuni ya Yas Tanzania, ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto.
Akipokea Vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali ameipongeza kampuni hiyo kwa harakati zake za kusaidia huduma mbali mbali za Kijamii.
Amesema, vifaa hivyo pia vitaweza kuimarisha huduma za mama wajawazito wanaofika hospitali hapo kupata huduma, Pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto katika hpspitali hiyo.
“Nyinyi sio tu watu wa mawasiliano kumbe muna upande mwengine ambao bado haujajulikana, sasa leo mmekuja kutuonesha mfano kwa kukabidhi baadhi ya hivi vitu ambavyo ni muhimu kwa Hospitali yetu na sehemu ya akina mama wajawazito,”amesema.
Amesema, Watoto wanapopata huduma nzuri, makuzi mazuri na afya bora, ndio watakaokua watumiaji wakubwa wa mitandao hiyo, huku hospitali ya kinyasini Pemba ikiwa ni ya tatau kwa kutoa huduma bora nchini.
Aidha amesema Vifaa hivyo walivokabidhiwa vitaweza kuongezea malengo yao ya utoaji wa huduma bora kwa jamii, huku akiwataka wafanyakazi wa YAS waliotoa michango yao kutambua kuwa wameekeza katika maisha yao, sambamba na kutambua kuwa Kampuni ya YAS ndio ya kuigwa.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wafanyakazi kuhakikisha wanavitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliokusudiwa, sambamba na kuwa kufanyakazi kwao kwa bidii ni moja ya sadaka muhimu katika maisha yao.
Mapema Mkuu wa Yas, Zanzibar, Mohamed Waqid ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongezwa na Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi, katika kuimarisha huduma za afya nchini Pamoja na kuhudumia huduma za kinamama wajawazito nchini.
Amesema, kupitia kampeni ya Tumaini, kampuni ya Yas imeona ikabidhi vifaa vitakavyoboresha huduma za uzazi kwa akinamama wajawazito wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
“Kampeni hii ya Tumaini ni yakipekee, kwani wazo lake limeanzia kwa wafanyakazi wenyewe baada ya kuguswa na changamoto zinazowakabili akinamama wanataka kujifua wanapofika hospitalini,”amesema.
Amevitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni Pamoja na Vitanda, viti Mwendo, vitanda vya kujifunguliwa, kanga, mashuka na vitu vyengine mbali mbali.
Hata hivyo amesema kamuni hiyo tayari imeshawafikiwa takriba wananchi asilimia 99% wa Zanzibar, kwa kuwapati huduma bora za kimtandao, kwani huduma na namna inavowajibika kwa jamii kila siku.
Nao baadhi ya akinamama walikuwepo Hospitalinih apo, wameishukuru kampuni ya Yas Tanzania, kwa misaada yao walioitoa hospitalini hapo.

More Stories
THTUB kuimarisha usimamizi wa haki,utawala bora
SGA yaimarisha utoaji huduma bora kwa wateja
Tanzania yajipanga kuvutia uwekezaji Mkubwa wa Nishati Duniani