Na Heri Shaaban, Timesmajira Online Ilala
HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa Amana,imeibuka kinara kati ya hospitali 28 katika utoaji huduma bora ya matibabu nchini,ambapo imekabidhiaa tuzo na Waziri wa Afya kwa Niaba ya Rais Samia, Aprili 8,2025.
Akizungumza katika hafla iliofanyika hospitalini hapo Katibu Tawala wa Mkoa Dar-es-Salaam Toba Nguvila,amesema hospitali hiyo, inatoa mchango wa kuisaidia Serikali kupitia Mganga Mkuu,amekuwa mbunifu na kuweka mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuiendeleza hospitali.

Amesema kwa sasa hospitali hiyo ina madaktari bingwa wa kisasa,wauguzi bora na vifaa vya kisasa huku akihadi kuwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Albert Chalamila,juu ya ombi la hospitali hiyo kuhusu kupatiwa eneo la Shirika la Nyumba.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana,iliopo wilayani Ilala, Brayson Kiwelu, amesema kupitia umoja wao wamekuwa wakifanya vizuri ngazi ya Mkoa,ambapo mwaka Jana waliandaa siku ya chakula cha usiku kwa ajili ya kuchangia moboresho ya miundombinu ya hospitali hiyo.
Ambapo kwa sasa wanaendelea kuboresha utoaji huduma ambapo Aprili 8,2025, wamepata tuzo ngazi ya kitaifa ,wanajipanga ili waweze kuchukua ya kimataifa.

Mjumbe wa Bodi ya hospitali hiyo Idda Luhanga ,amesema, mikakati yao wachukue tuzo zote kila mwaka hivyo watachukua maoni ya wateja kupitia sanduku la maoni.
More Stories
Wenyeviti Ilemela wafunguliwa macho kuhusu wahamiaji haramuÂ
Wadau waitwa kuchangia upauaji Maabara sekondari ya Mtiro
Coca-Cola yazindua Kampeni ya ‘Chupa la Machupa’