December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hospitali Rufaa Kanda ya Mbeya yapokea hundi ya milioni 37.5

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

UMOJA wa wafanyakazi wanawake wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya umekabidhi hundi yenye thamani ya zaidi milioni 37.5 kwa ajili ya ununuzi wa kitanda cha kisasa cha upasuaji wa mifupa wa hospitali hiyo.

Akipokea hundi hiyo Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya ,Dkt. Godlove Mbwanji ameshuru na kuupongeza Umoja wa Wanawake Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kuwa chachu na mchango mkubwa katika maendeleo ya Hospitali na mkoa kwa ujumla.

Dkt.Mbwanji amesema kuwa wanawake hai ni chachu kubwa kwa mafanikio ya hospitali na mkoa kwa ujumla na kuwapongeza wanawake wote Tanzania nzima kwa mchango mkubwa wa maenedeleo ya nchi .

Hata hivyo Dkt . Mbwanji amewataka wanaume kuweka jitahada zaidi katika malezi ya mtoto wa kiume ili kujenga taifa lenye vijana imara katika jamii.

“.Lakini sasa hebu tuwatazame watoto wa kiume na hii sio kwa akina mama ni kwa upande wa akina baba pia ili mwisho wa siku tuwe na taifa lenye vijana imara hivyo Ndugu zangu wanaume tuna kila Sababu za kujikita katika malezi ya watoto wetu wa kiume ili kuwa na Taifa lenye kizazu.chenye manufaa “amesema Mbwanji.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo Katibu wa Umoja wa Wanawake katika hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya , Joyce Komba amesema lengo la kukabidhi zawadi hiyo ni kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na kuushukuru uongozi hiyo kwa kuwaongoza katika misingi imara inayopelekea kutoa huduma bora kwa wagonjwa na kudumisha umoja, upendo na mshikamo.

Dkt. John Mbanga ni Mkuu wa Idara ya Upasuaji hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ameshukuru kwa zawadi hiyo na kusema upatikanaji wa kitanda hicho umekuwa msaada mkubwa sana hasa katika kipindi ambacho ajali zimekuwa nyingi na kusema kitasaidia kurahisisha huduma ya upasuaji wa mifupa.

“Jambo.lilofanywa na wanawake Hawa limenigusa sana na zawadi hii maana imekuwa ni kilio kikubwa sana kwa idara ya upande wa mifupa kama tunavyojua kwa sasa ajali zimeongezeka hivyo kitanda hiki kitakuwa msaada mkubwa. Kwa wagonjwa wetu na tunazidi kupongeza juhudi kubwa hizi zilizofanywa na wanawake Hawa kwani wamefanya jambo kubwa “amesema ” Dkt.Mbanga

Katika hafla hiyo fupi , Umoja wa Wanawake Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ulipata nafasi ya kumkabidhi tuzo ya hesima Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha shughuli mbalimbali
Katika umoja huo na hospitali kwa ujumla.

Umoja wa Wanawake Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ulianza mnamo mwaka 2022 ukiwa na wanachama 400 na hadi kufikia mwaka 2024 unaongezeko la wanachama 209 unaojumuisha wanawake mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali ndani ya hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.