Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online Dar
IDARA ya Ustawi wa Jamii ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU) kwa kushirikiana na Hospitali ya Kairuki wameandaa kambi ya mwezi mzima kwaajili ya kutoa ushauri na elimu ya afya ya akili.
Huduma hiyo inatolewa bure katika viwanja vya maegesho Mlimani City jijini Dar es Salaam na itaendeshwa kwa mwezi mzima wa Julai kwa siku za Alhamis, Ijumaa na Jumamosi.
Mkufunzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii wa (HKMU), Esther Katende, ameiambia TimesMajira,Online leo kuwa wameona watoe huduma hiyo baada ya kubaini kuwa tatizo hilo linazidi kuongezeka.
“Tumeona ni vyema kuandaa mwezi wa afya ya akili baada ya kuona tatizo linaongezeka na matukio mengi ya mauaji yanazidi kushamiri sehemu mbalimbali nchini hivyo tumeona jamii inahitaji huduma muhimu ya
ushauri, “ amesema
Aidha, amesema mbali na kutoa huduma ya afya ya akili na ushauri pia wanapima afya kwa ujumla kwa watu wote watakaojitokeza kwenye kambi hiyo na kuwapa ushauri wa kitaalamu wale watakaokutwa na shida mbalimbali.
“Viashiria vya tatizo la afya ya akili viko vingi, mojawapo ni kujitenga au kutengwa, ukimya usio wa kawaida, mabadiliko katika mtiririko wa mawazo, maongezi na matendo hivyo basi viashiria hivi vikionekana kwa mtu awahishwe kwa wataalam ili kupata msaada mapema,”amesema
“Idara ya Ustawi wa Jamii ya Hubert Kairuki Memorial University pamoja na vyuo vingine vinavyotoa elimu ya Ustawi wa Jamii ni chimbuko mojawapo la wataalam wanaotoa huduma kwa wagonjwa wa aina hiyo, ”amesema Esther
Aidha, aliwakaribisha watu wote kupata ushauri na elimu kuhusu afya ya akili pamoja na upimaji afya katika viwanja hivyo vya maegesho Mlimani city Mall ili waweze kufahamu vyema kuhusu afya zao ili kama
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango