Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Maalum,TAMISEMI, Ernest Hinju ametoa agizo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwapatia vifaa saidizi Walimu wenye ulemavu ili waweze kufurahia kazi yao wakati wa ufundishaji wa elimu jumuishi.
Hinju amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa “Peleka Rafiki zangu Shule” wenye thamani ya zaidi ya bilioni 2,unaolenga kuendelea kutoa mafunzo ya elimu jumuishi kwa walimu.
Uzinduzi huo umewashirikisha wadau wa elimu kutoka mikoa ya,Songwe,Rukwa na Katavi pamoja walimu wanaofundisha elimu jumuishi,walimu wa kujitolea kutoka mikoa ya Songwe,Katavi uzinduzi huo umefanyika Gr hoteli iliyopo jijini hapa.
Hinju amesema kuwa TAMISEMI imekuwa ikipata taarifa kwamba kuna baadhi ya walimu wenye ulemavu hawasaidiwi vifaa saidizi shuleni ili waweze kukaa sawa wakati wa ufundishaji hali inayowafanya walimu hao kufanya kazi katika mazi
Kwani wamekuwa wakipokea simu kutoka kwa walimu wenye ulemavu wakiomba uhamisho wa kuhamia mjini na kwamba wakifanya hivyo elimu jumuishi haitakuwepo na wakianza kutengana kwa hali hiyo haitasaidia chochote na kuwataka wakurugenzi wajitahidi kuwasapoti pamoja na kuonyesha nia.
“Nitoe wito kupitia Maofisa Elimu mliopo hapa pelekeni salamu ziwafikie wakurugenzi wote nchini kupitia jukwaa hili kwamba kwa mujibu wa taratibu na wajibu wa muajiri ana wajibu kumpatia vifaa saidizi mwalimu mwenye ulemavu ili aweze kukaa sawa najua kuna changamoto ya kibajeti lakini wajitahidi walau kila mkurugenzi aonyeshe nia hata kile kidogo anachopata,”amesema Hinju.
Akizungumzia kuhusu watoto wenye ulemavu waliofaulu kutoripoti kidato cha kwanza Hinju amesema kuwa Februari mwaka huu walifanya ufuatiliaji na kugundua kuna wanafunzi 143, hawajaripoti kuanza kidato cha kwanza na katika hali hiyo aslimia 4.6 pekee wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza huku 95 wamefanikiwa kuripoti shule.
“TAMISEMI tumeelekeza wakurugenzi kupitia Maofisa Elimu Maalum wahakikishe hakuna mtoto mwenye ulemavu ambaye hajaripoti shule na kama ana changamoto ni wajibu wa Halmashauri kusapoti ili changamoto hizo zisimkwamishe kuanza masomo vinginevyo jitihada za kuwainua watoto hawa zitakuwa hazina maana,lakini cha kusikitisha unampigia simu Ofisa Elimu Maalum hatoi ushirikiano,”amesema Hinju.
Mkurugenzi wa Child Support Tanzania (CST) Noela Msuya amesema mradi huo utahudumu kwa muda wa miaka minne huku akitaja hatua kadhaa zilizotekelezwa na mradi huo tangu kuanza kwake mwishoni mwaka mwaka jana unafadhiliwa na serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na CBM unatekelezwa na shirika hilo.
Ambapo ameeleza kuwa umefanikiwa kuwafikia watoto zaidi ya 1000 huku zaidi ya shule 50 zikinufaika na mafunzo ya elimu jumuishi.
Mafunzo ya elimu jumuishi yatawasaidia wazazi,walezi na jamii katika kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu haki ya elimu hususani kwa watoto wenye ulemavu.
Pamoja na hayo Msuya ametaja changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya elimu jumuishi ikiwemo miundombinu isiyo rafiki kwenye shule mbalimbali,upungufu wa wataalamu wa elimu jumuishi na changamoto ya mitihani kwa watoto wenye ulemavu huku akiomba serikali kuagalia changamoto hizo kwa jicho la pili.
Kwa upande wake Meneja Miradi wa Taasisi ya Child Support Tanzania (CST)Nemesi Temba amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa mikoa mitatu ambayo ni Songwe,Katavi na Rukwa na kuwa lengo la mradi huo ni kuongeza idadi ya elimu jumuishi kwa mikoa hiyo.
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi