November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hilda:Uelewa juu ya usonji umeongezeka

Na Mwandishi wetu, timesmajira

IMEELEZWA kuwa uelewa katika jamii kuhusu usonji umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na elimu inayotolewa kwa jamii tofauti na miaka ya nyuma, ambapo imesaidia watoto wengi kutofungiwa ndani.

Kauli hiyo ilitolewa leo Jijini Dar es salaam na Mwanzilishi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Lukiza Autism foundation
Hilda Nkabe wakati alipotembelea Shule ya Msingi ya Msimbazi Mseto kitengo cha watoto wenye usonji kwa ajili ya kujumuika nao pamoja katika kuadhimisha siku hiyo.

Amesema kwa sasa jamii inauelewa wa kutosha tofauti na miaka ya nyuma kwani wazazi na walezi wameweza kuelewa na kuwatambua mapema watoto hao wenye usonji.

“Licha uelewa kuongezeka ..bado vijijini elimu ni ndogo kutokana na baadhi ya watu kuhusisha na Usonji na imani za kishirikina hivyo bado tunaendeleza elimu”amesema Hilda

Aidha amesema hali ya jamii kuanza kukubali usonji k kumeanza kuonekana kwa kiasi jambo ambalo limesaidia kupunguza kuchekwa, kuziaki na kubezwa.

Vilevile amesema ipo haja ya kuwa na kituo jumuishi ambao kitasaidia kupatikana kwa elimu sehemu yoyote ili kuondoa changamoto ya watoto wanaoishi au kutoka mbali.

Mkurugenzi huyo ambaye nae ni mama wa mtoto wenye Usonji alisema ulezi wa watoto wenye usonji sio wa mtu mmoja bali ni wajamii nzima.

“Mimi nilijua chagamoto ya mtoto wangu mapema tangu akiwa na miaka miwili na nusu hii ilinisaidia kumjua mtoto mapema na kuweza kumsaidia pia ilinipa mda wa kukubali hali yake “amesema Hilda

Aidha ameema Serikali imeweza kusikia kilio cha watoto wenye usonji ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika elimu na mazoezi tiba.

“Tunamshukuru Serikali Kwa kuendelea tuunga mkono ila tuniomba iweze kuongeza shule kwa ajili ya watoto wenye usonji pamoja dawa”amesema

Pia amesema licha ya kuwepo jwa uelewa katika jamii ni muhimu kuanza kufanyika kwa tafiti juu ya chanzo Cha ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuanza kulifanyia kazi dhana zinazotajwa.

Kwa upande wake Daktari kutoka Taasisi ya AfyaCheck ambao ni wasimamizi huduma kwa watoto wenye usonji waliopo shule mbalimbali ikiwemo Msimbazi Mseto Isaac Maro alisema usonji ni hali ambayo utokea Kwa mtoto na kuishi maisha yake yote .

“Hali hii uwa na viashiria vikuu vitatu ikiwemo mawasiliano, ushidwaji wa kuchagamana vizuri pamoja na kuwa na tabia za kujirudiarudia hivi ndivyi viashiria vikuu vinavyoonekana kwa watu wenye usonji”amesema

Amesema Hali hiyo kuonekana kwa watoto kuanzia miezi sita mpaka miezi 18 huku ikitegemewa ukaribu wa mtoto na mzazi

Naye mzazi wa mtoto mwenye usonji alisema Mecktrida Mtaki aliipogeza Taasisi ya Lukiza Autism foundation kwa kuwaunganisha na watoto wengine kujifunza mambo