January 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hawa amlilia Rais Samia

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Mwananchi wa Maputo MBWENI wilayani Kinondoni, HAWA BEDUI , anamlilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, aweze kumsaidia Katika mtaa wa Maputo ,mbweni shina namba tatu anataka kuporwa sehemu ya ardhi yake na Mwekezaji anaye miliki zaidi ya heka 70 eneo hilo .

Hawa Bedui ,alitoa kilio hicho leo wakati wa kuongea na waandishi wa habari kuomba kilio chake Rais aweze kukisikia amsaidie haraka baada kuzuiwa kufanya ujenzi sehemu ya eneo Lake kufuatia mwekezaji huyo kuvamia na mabaunsa kuvunja eneo la hawa kinguvu akidai ni sehemu yake

“Rais Samia suluhu Hassan mwanamke mwezangu naomba nisaidie ili haki iweze kutendeka mimi ndio mmiliki wa eneo hili tuko toka mwaka 1999 ndio tumenunua eneo hili tukipakana na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania marehemu Daudi Balali ,ndio alikuwa jirani yangu nimeshaangaa baada Balali kufariki ametokea mwekezaji amedai eneo langu lipo kwake amekuja na greda amevunja ” alisema Hawa.

Hawa alisema awali mwekezaji huyo alifika katika eneo Lake akamshauri ampe shilingi 200,0000/=aweze kumchongea na greda hawa akatambua ni mtu mwema ilipofika Agosti 31 mwaka huu walifika mabaunsa na greda wakavunja sehemu ya eneo lake bila ya maelewano yoyote.

“Sehemu hii eneo langu mipaka michongoma na mkonge ,pia bikoni zimewekwa toka mwaka 1999 mpaka sasa baada kuvunjwa ukuta shauri limepelekwa Baraza la Kata kila akiitwa katika kikao cha Baraza ajawai kutokea mpaka sasa “alisema

Mjumbe wa shina namba 3 Mbweni Maputo wilayani Kinondoni ,Damas Mashaka alisema ,eneo hilo analifahamu toka mwaka 2004 mgogoro huo anaifahamu vizuri Agosti 31 mwaka huu huyo mwekezaji alifika akidai eneo la barabara wakati sio kweli mkonge ulikuwepo muda mrefu huyo mwekezaji alifika na kuzuia mafundi wasijenge.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Maputo Mbweni ,Mazoea Matope alisema,ameingia madarakani mwaka 2019 na eneo hilo analifahamu kila mwaka lina michongoma na mikonge baada mwekezaji kuvamia eneo hilo alipokea shauri hilo na kumshauri apeleke malalamiko yake baraza la Kata Mbweni kwa ajili ya utatuzi wake