January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Harmonize, Mzee Yusuph kufanya ‘Colabo’ ya taarabu

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Kondegang hapa nchini, Rajabu Abdul maarufu ‘Harmonize’ amesema yuko mbioni kuachia wimbo wa taarab ambao atamshirikisha nguli wa muziki huo Mzee Yusuph.

Licha ya kuweka wazi jambo hilo lakini pia msanii huyo aliimba kionjo cha wimbo huo ambao anauandaa na ukikamilika atamshirikisha Mzee Yusuph.

Hiyo imekuja, baada ya hivi karibuni Mzee Yusuph kuweka wazi kuwa anatarajia kurejea kwenye muziki huku akiwataka watu wakae mkao wa kula ataibuka na kitu gani.