December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Harmonize aombwa kuondoa tatuu ya Sarah

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MASHABIKI wa msanii wa muziki wa Bongo fleva, Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize, wamemuomba mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ‘Anajikosha’ afute tatuu ya aliyekuwa mkewe, Sarah.

Hatua hiyo imekuja, baada ya Sarah kumuanika mpenzi wake mpya na kumuita ‘My Love’ kuonesha kwamba hakuna uwezekano wa wawili hao kurudiana huku hakiweza wazi kuwa ana mwenza mwengine.

Tatuu ya jina la Sarah bado ipo kwenye mkono wa kulia wa Harmonize, licha ya wawili hao kuachana mwaka jana kwa tuhuma za usaliti ambapo jamaa huyo alitua kwa Kajala Masanja ambaye naye wameachana.