Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Kondegang Rajabu Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ amemtumia ujumbe mzito aliyekuwa mpenzi wake msanii wa filamu hapa nchini Kajala masanja na wanawake wengine aliyewahi kutembea nao, kupitia wimbo wake mpya ‘Vibaya’ ili waendelee kuishi kwa amani licha ya wawili hao kuachana.
Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagrama mara baada ya kutoa wimbo huo Harmonize amesema, kutoka kwenye moyo wake siku zote ataendelea kumuheshimu kila mwanamke aliyewahi kuwa katika mahusiano na yeye kwani ndio waliomfanya akawa Harmonize.
“Kutoka kwenye moyo wangu, ni ukweli usiofichika nilianza na Jack baadaye Sarah kisha Kajala, kila mmoja kwa wakati wake. Na kwa hakika hawa ndio wanawake walionifanya leo hii nikawa ‘Harmonize’, kwa pamoja tumepitia mazuri mengi na mabaya,pia mara nyingine siziangalii tofauti pekee, naangalia zaidi nyakati za furaha tulizopitia ndia maana sijawahi kumdharau au kumuongelea vibaya yoyote kati yao.
“Isitoshe kusema nawaheshimu na kuwathamini na naamini ni zaidi ya marafiki na ndugu niliowahi kuwa nao. Tofauti hutokea muda wote bila kujali ni za aina gani au zinatokea wapi, ila moyoni naamini haziwezi vunja upendo tulio utengeneza kwa muda mwingi. Siku zote nitaendelea kuwapa kipaumbele kama wanawake wenye nafasi kubwa sana kwangu, ukiacha Mama yangu mzazi, ningependa kuwaona wenye furaha ili hata kesho na kesho kutwa tuje kuzikana maana hakuna aijuae kesho yake.
“Naamini kuachana ni mwisho tu wa maridhiano kutokana na sababu husika lakini sio vita wala uhasama!, au ikiwa chanzo cha kudhalilishana na nisingependa kuongea zaidi kuhusu Kajala, ambae naweza sema ndio mtu wa mwisho kumiliki moyo wangu. Leo tupo wazima lakini hakuna anayeijua keshom haina sababu ya kuoneshana nani zaidi, nani kaumia au nani kakosea zaidi kiliko mwengine, kwani haina maana yeyote lakini pia ni kuwapa ushindi watu waliokuwa wakipambana na kuona haya mahusiano hayapo tena.
“Kama ilivyo ada nitaendelea kukuheshimu na kukuombea mafanikio mema, umekuwa mtu mzuri kwangu hususani kwa kipindi tulichokuwa pamoja. Kwa kuwa mimi sio mtu wa kuelezea elezea sana, ilikuwaje, ikawaje, nafunika kombe mwanaharamu apite lakini pia niwashukuru Engineers wote mliofanikiwa kulikamilisha hili, ni plani nzuri na imefanikiwa. Ila niombe tu iwe kwa amani, isiwe ‘Vibaya’,” ameandika Harmonize.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA