Judith Ferdinand,TimesMajira Online,Mwanza
Halmashauri za Mkoa wa Mwanza zimetakiwa kuwapatia mikopo vijana waliopatiwa mafunzo na shirika lisilo la kiserikali la Plan International ili waweze kuendeleza miradi waliyoanzisha.
Hayo yameelezwa na Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza Janeth Shishila
katika warsha ya kufunga mradi wa Vijana,Maisha na Kazi uliokuwa ukiendeshwa na Shirika la Plan International kwa kushirikina na taasisi za kiserikali kwa vijana wa Wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza.
“Naagiza halmashauri wanakotokea vijana hawa kuhakikisha wanawapatia mikopo ili kuendeleza miradi yao ambayo tayari wameianzisha.,”ameeleza Janeth.
Pia amewataka vijana hao waunganishwev na vijana wengine ili kupeana ujuzi na uzoefu wa biashara mfano kuna vikundi ambavyo wana bidhaa tofauti na wanazozalisha vijana hao wawe wanabadilishana bidhaa kama unatengeneza sabuni na mwingine batiki ili kisaidiana kutafuta masoko.
Kwa upande wake Meneja wa shirika la Plan International Mkoa wa Mwanza Majani Rwahambali ,amewaomba viongozi wa serikali katika ngazi za kata na vijiji kuwasimamia vijana hao ili waweze kutumia vifaa walivyopewa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Huku akiwataka vijana hao kuvitunza vifaa hivyo pamoja na kuendeleza miradi waliyoanzisha kwa faida yao na jamii kwa ujumla.
“Maofisa watendaji na maendeleo katika mitaa na kata zetu na hata wenyeviti wa mitaa wawasimamie vijana hawa ikiwezekana wasajili hivi vifaa tulivyowapa ili vifanye kazi iliyokusudiwa maana hata wengine wanaweza wakavutumia kwa uhalifu mfano mashine za kukatia alluminium,”ameeleza Majani.
Ambapo miongoni mwa tasisi za serikali zilizoshirikishwa ni Sido ambao wamefanikisha utoaji wa mafunzo pamoja na mikopo kwa vijana hao licha ya kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi yao kushindwa kumaliza mafunzo.
Meneja Mradi wa Vijana Maisha na Kazi, kutoka shirika la Plan International Gadiely Kayanda ameeleza kuwa mradi huo umefanikiwa kufikia lengo la kuwawezesha vijana kupata mitaji, kujiajiri, kuwaunganisha na sekta binafsi pamoja na kuwajengea usawa.
“Vijana hawa wamepata mafunzo katika fani mbalimbali ikiwemo ufuaji vyuma, upishi, mapambo, ushonaji, useremala, ufundi mabomba na ujenzi tayari wamepewa mtaji wa vifaa kulingana fani na ujuzi wao na kukabidhiwa mikononi mwa Serikali kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii na maofisa vijana katika halmashauri zao kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji,”ameeleza Kayanda.
Ofisa Kilimo kutoka Taha, Reymond Gervas
ameeleza kuwa licha ya changamoto kadhaa ikiwemo ya vijana wengi kutomiliki mashamba, mafunzo ya kilimo bora yamenufaisha vijana 412 na kuvuka lengo la awali la kufikia vijana 400.
Mkufunzi kutoka Sido, Maporo Maneno ameishukuru Plan International kwa kuwezesha ujenzi wa jengo lenye mashine za kusindika vyakula na kuchakata kemikali kwa gharama ya zaidi ya milioni 70,ambapo jengo na mashine itawanufaisha vijana wote hata ambao hawakuwemo kwenye mradi.
Miongoni mwa vijana walionufaika na mradi huo Victor Herman ameeleza kuwa kwa sasa amejikwamua kiuchumi na kuwakwamua wengine.
” Mimi Kwa sasa katika kikundi cheti cha msitu ni uhai tumefanikiwa kujikwamua kiuchumi kutokana na elimu tuliyopata ya namna ya kutunza fedha tunazopata na sasa tunaweza hata kukopeshana wenyewe fedha tunazozalisha katika mradi wetu,”ameeleza Herman.
Mradi wa vijana maisha na kazi uliotekelezwa na shirika la plan international kwa kushirikiana na Tanzania Hotculture Association (TAHA),Veta na Sido ulikuwa na lengo la kumwezesha kijana kupata mtaji,kujiajiri,kuleta usawa wa kijinsia pamoja na kuwaunganisha vijana na mashirika mbalimbali.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza Janeth Shishila akizungumza na washiriki wa warsha ya kufúnga mradi wa kijana,maisha na kazi,hawapo pichani.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya kufunga mradi wa kijana,maisha na kazi
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano