Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Rukwa
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi imepokea boti kutoka Wizara ya Afya ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha utoaji wa huduma za afya hususani utoaji chanjo katika maeneo yaliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika.
Kupatikana kwa boti hiyo kutarahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za afya ikiwemo usambazaji wa chanjo, usimamizi wa huduma za chanjo pamoja na utoaji wa huduma mkoba katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika.
Ambapo hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha watoto na wananchi kwa ujumla wanaoishi katika maeneo ya mwambao mwa ziwa Tanganyika,wanapata huduma bora za kinga dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo na kuboresha usimamizi wa huduma hizo kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi,Afraha Hassan,amesema,kulingana na mazingira ya ukanda wa ziwa Tanganyika jiografia ya maeneo hayo ni ngumu,hali inayochangia wagonjwa kushindwa kupata huduma za afya za uhakika hasa zile za dharura na chanjo,hivyo kupitia boti itakuwa suluhisho kwa changamoto hiyo.
Licha ya boti hiyo iliyotolewa na serikali kujikita zaidi katika eneo la chanjo pia itatumika kubebea wagonjwa wa dharura “ambulance”,kwa ajili ya kuwapeleka katika vituo vya afya au kwenye hospitali zenye huduma zaidi.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina