November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halmashauri ya chamwino yawaita wanawake wenye mahitaji ya uwezeshwaji

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Halmashauri ya Chamwino Jijini Dodoma imewataka wanawake ambao wana mahitaji hasa ya mitaji kutumia halmashauri hiyo pamoja na wataalamu wake ili waweze kufika katika kiwango kikubwa cha uzalishaji

Mbali na kutumia wataalamu pamoja na kutumia Halamshauri hiyo,bado wanaopewa mahitaji ikiwemo mitaji nao wanatakiwa kuwa waaminifu ili na wengine waweze kunufaika

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodomana mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya chamwino Bw Edson Jeradi Sweti wakati akiongea Kwenye kikao cha Actionword kwa ajili ya majukwaa ya wanawake

Bw Edson alisema kuwa wao kama halmashauri wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wanawasaidia wanawake kwani wanawake ambao wamesaidiwa na halamshauri hiyo wameonesha matokeo makubwa hasa kwenye uzalishaji

Ameongeza kuwa kwa wanawake ambao wameshapata Mitaji na elimu ya utaalamu hiyo wamefanikiwa kupata faida sana na wameongeza uzalishaji na vipato kuanzia ngazi ya familia hadi ngazi za juu

Katika hatua nyingine alisema kuwa bado wapo baadhi ya wanawake ambao wanapewa mikopo na uwezeshwaji kutoka katika halmashauri hiyo lakini bado wameshindwa kukidhi vigezo

“nimekuwa nikipokea taarifa kuwa wapo ambao wanadanganya wanajishugulisha na kitu Fulani lakini ukija kuwana kagua hilo linakuwa halipo,mimi na Mkurugenzi wangu huwa hatuwaachi hawa wakina mama tunawatembelea wote

Nao baadhi ya wanawake ambao wameshiriki katika Baraza hilo walisema kuwa halmashauri hiyo imekuwa msaada mkubwa sana kwa kuwa imewapa Mitaji ambayo imewakomboa na kuachana na umaskini ambao umekithiri kwenye jamii

Wanawake hao walitoa wito kwa wanawake wengine nchini kuhakikisha kuwa wanawatumia wataalamu wa halmashauri pamoja na mikopo ambayo inatolewa kwa kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita inataka kila mwanamke awe na maendeleo.