Na Esther Macha, Timesmajira, Online,Masasi
UANZISHWAJI wa shule mpya ya msingi ya mkondo mmoja Mkomaindo iliyopo katika mtaa wa Darajani utapunguza msongamano wa wanafunzi,utoro pamoja na kutembea umbali mrefu wa kwenda shule mama ya awali.
Imeleezwa kuwa baada ya vikao vya kamati mbalimbali ambavyo vilihusisha wananchi waliamus kuwa shule hiyo ijengwe mtaa wa Darajani ili kusogeza huduma za kijamii na hasa ukizingatia kuwa Kata hiyo ina shule moja tu.
Hayo yamesemwa na Mwalimu Mkuu wa shule Mama Mkomaindo ,Suzan Mwaya wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Masasi alipofanya ziara ya kutembelea shule tatu zinazojengwa kwa mradi wa Boost.
Ambapo ameeleza kuwa shule ya Mkomaindo ilipatiwa zaidi ya mil.331 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya yenye mkondo mmoja.
Mwaya amesema kuwa shule hiyo kwasasa ipo kwenye hatua za umaliziaji vimebaki vitu vichache na kwamba walipata changamoto kubwa kwenye matundu ya vyoo vya wanafunzi ya awali kwani walishauriwa kuwa hayako sehemu sahihi ikabidi yafukiwe na kuchimbwa sehemu nyingine.
“Namshukuru sana Rais Samia kwa kutuona hata sisi tuliopo pembezoni mwa Tanzania na kuona matatizo tunayopata kwenye uwezeshaji katika sekta ya elimu ,shule ya msingi Mkomaindo ina wanafunzi wengi ambao ni 1,531 kiasi kwamba unakuta darasa moja wanakaa watoto 185 hivyo kushindwa kumfikia hata yule mtoto aliyemwisho kabisa,”amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Masasi Erica Yegella amesema kuwa ahadi kubwa watakapopata fedha hata kama ni mapato ya ndani wataongeza vyumba vya madarasa maana watoto ni wengi inaweza kujengwa hata mikondo miwili.
Aidha Yegella amesema kuwa Mdhibiti Ubora wa shule akikubaliana na shule wataleta walimu wa kutosha ili kazi iendelee .
“Mwalimu Mkuu wa shule na Diwani mmefanya kazi kubwa ya kusimamia ujenzi wa shule hii naamini itakuwa mkombozi kwa watoto wetu namshukuru S Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutuona wana Masasi naamini sasa watoto watasoma vizuri hata ule umbali waliokuwa wakitembea kwenda shule hautakuwepo,”amesema Mkurugenzi Yegella.
Diwani wa Kata ya Mkomaindo ,Ally Salvatory amesema kuwa shule ya mama Mkomaindo ina watoto 1,531 ndio chimbuko la mgawanyo mpaka ikajengwa shule mpya na kuwa jumla ya wanafunzi 700 wataletwa kwenye hiyo mpya kutoka shule Mama ili watoto waweze kusoma .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba