Na Mwandishi wetu,Timesmajira,Online
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM inatarajiwa kukutana Jumanne Juni 22, 2021 chini ya Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo mkoani Dodoma na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Shaka Hamdu Shaka amesema kikao hicho kimetanguliwa na kikao cha SeKretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Amesema kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa NEC White House Jijini Dodoma na kuikutanisha Sekretariet hiyo ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Kamati kuu.
“Ni kweli Jumanne 22 Juni 2021 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ataongoza kikao cha kawaida cha kamati Kuu, maandalizi yote yamekamilika, ni kikao cha kawaida cha Kikatiba”amesema Shaka
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua