January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halmashauri Jiji la Dar waibuka kidedea kilimo Kanda Mashariki

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Morogoro

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam WAIBUKA KIDEDEA katika maonyesho ya wakulima nanenane Kanda Mashariki Morogoro.

Akikabidhi tuzo hizo katika kilele cha maonyesho ya nane nane Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Bunge George Simbachaweni alisema Halmashauri ya Jiji imeibuka wa kwanza kwenye kundi la Halmashauri za Miji na manispaa kwa mwaka 2022.

“HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa ya kwanza kwenye kundi la halmashauri za Miji na manispaa nane nane Kanda Mashariki Mwaka huu 2022 “alisema Simbachaweni.

Akizungumzia Maonyesho hayo ya Kanda Mashariki Waziri Simbachaweni alisema maonyesho ya nane nane yawe kitovu bila kusahau kuitangaza sekta ya uvuvi .

Alisema Serikali itashirikiana na wadau Kanda Mashariki VIWANJA vya nane nane maonyesho yatakuwa yakitaifa .

Alitoa rai viwanja hivyo viboreshwe kwa wadau wa maendeleo na Mamlaka za Serikali kuchukua hatua na wadau wapewe kipaumbele

Mkuu wa Idara ya Kilimo na Uvuvi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Majaliwa Andrew alisema katika Halmashauri 24 kati ya 20 Ilala imeibuka ya kwanza na katika mkoa wa Dar es Salaam Halmashauri ya Jiji pia imeomgoza .

Mwenyekiti wa Huduma za Jamii Halmadhauri ya Jiji Steven Mushi alisema Halmashauri yetu umefanikiwa katika mambo mengi imeshika nafasi ya kwanza katika usafi pamoja na UMITASHUMTA Tabora.

Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Madiwani,WAkuu wa Idara na Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Jiji kuviwezesha vikundi mikopo ya asilimia Kumi ya Wanawake Vijana na Watu Wenye Ulemavu .

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Bunge George Simbachaweni akimkabidhi kikombe na cheti Mkuu wa Idara ya Kilimo na Uvuvi Halmashauri ya Jiji Majaliwa Andrew katika maonyesho ya Wakulima Nanenane Kanda Mashariki Morogoro (kushoto)Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatuma Mwasa (Picha na Heri Shaaban )
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Uvuvi Halmashauri ya Jiji Majaliwa Andrew akimkabidhi kombe na vyeti Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija kufuatia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuibuka washindi wa kwanza kwenye kundi la Halmashauri za Miji zilizoshindanishwa katika maonyesho ya Wakulima Nanenane Kanda Mashariki Morogoro Agosti 08/2022 (Katikati)Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Charangwa Selemani (PICHA NA HERI SHABAN)