Alexei Navalny ambaye ni Mwanasiasa wa upinzani hana fahamu akiwa hospitalini kutokana na kile kinachoshukiwa kuwa ameathirika na sumu, msemaji wake ameeleza.
Mpiga kampeni dhidi ya vitendo vya rushwa alianza kujisikia mgonjwa alipokuwa safarini kwenye ndege, hali iliyofanya ndege aliyokuwa akisafiri nayo kutua kwa dharura mjini Omsk, ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa hana fahamu na walikuwa wakijaribu kuokoa maisha yake.
Timu yake inashuku kuwa kuna kitu kiliwekwa kwenye chai katika mgahawa wa uwanja wa ndege .
Ikulu ya Urusi imesema inamtakia ”afya njema na ya haraka bwana Navalny”
Bwana Navalny, 44, kwa miaka mingi amekuwa mmoja kati ya wakosoaji wakubwa wa Vladimir Putin.
Mwezi Juni alieleza kuwa kura ya mabadiliko ya katiba ni ”mapinduzi” na ”ukiukaji wa katiba”. Mabadiliko yanampa fursa Putin kuongoza tena mihula miwili, baada ya minne aliyokuwa nayo.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab amesema kuwa ”amesikitishwa sana” na ripoti kuwa alikuwa amepewa sumu, na kutuma salamu za pole kwake na familia yake.
Taasisi ya German Peace ina matumaini ya kutuma ndege ya kusafirisha wagonjwa ili kumchukua Navalny kuelekea Berlin kwa ajili ya matibabu.
Hospitali ya Charite mjini Berlin iko tayari kumtibu, Jaka Bizilj , Mkurugenzi wa mfuko huo ameeleza.
”Tuko kwenye mazungumzo na mamlaka na kuna matumaini kuwa vibali vyote vya usafiri na ripoti za kitabibu zitapatikana usiku huu.” aliongeza.
More Stories
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Samia avuna makubwa Mikutano ya Uwili G20
Dk. Mpango amwakilisha Samia sherehe za Uhuru wa Lesotho