January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Haji Manara ateuliwa kuwa balozi wa pikipiki za hunter

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MDAU wa soka nchini, Haji Manara ameteuliwa kuwa balozi wa pikipiki za hunter zinazozalishwa na kampuni ya Hero na kusambazwa na Sunbeam Auto Ltd

Akizungumza na Waandishi wa Habari akiwa kwenye ofisi za kampuni hiyo leo Jijini Dar es salaam, Manara alibainisha kuwa atatumia ubalozi wake huo katika kuwasaidia waendesha bodaboda kuepuka ajali za barabarani na hasa katika kuwaelimisha masuala mbalimbali kuhusiana na ajali hizo za barabarani.

Alisema imekuwa ni kawaida kwa waendesha bodaboda kuendesha usafiri huo bila ya kuvalia kofia ngumu za kuwakinga na madhara ya majeraha pindi ajali ikitokea huku akisisitiza kuwa katika kila kona ya nchi atakayokuwa akienda kufanya kazi ya ubalozi wake huo atajikita pia katika kutoa elimu ya kuwasaidia waendesha bodaboda kujilinda dhidi ya ajali.

‘’Kwa hatua hii ya bodaboda za Hunter kutoa kofia ngumu yani hizi helmet mbili kwa kila bodaboda moja wanayouza kwa ajili ya mwendesha bodaboda na abiria, ni hatua nzuri na yenye kuonesha nia ya dhati ya kuwanusuru dhidi ya majeraha, hivyo kwangu nikiwa balozi mbali na kuzitangaza nitatangaza umuhimu wa kutii sheria za usalama barabarani’’ alisema Manara.

Alisema kuwa bei za bodaboda ambazo ni hunter 100 CC, 125 CC na hunter 150 CC zinazofanya kazi kwa kauli mbiu ya piga gia barabara ishangae inayoelezea ubora wa pikipiki hizo zinapatikana nchini nzima kwa mawakala 27 huku ikiwa na bima hadi ya Sh million tano na huduma ya ukarabati mara tatu za mwanzo.

Kampuni ya Hero MotoCorp inaongoza kwa kutengeneza na kuzalisha pikipiki zinazoongoza kwa ubora duniani ambapo kwa Hunter 100CC inauzwa kwa Sh milioni 2.45, na Hunter 125CC- inayouzwa kwa Sh milioni 2.50 huku Hunter 150CC ikiuzwa kwa Sh millioni -2.90. Pamoja na hayo kuna fursa za mikopo kwa wanaohitaji.

“Vipuri vya pikipiki hizi vinapatikana kila kona ya nchi kwa ajili ya kuwawezesha wateja wetu kuwa na uhakika wa kufanya matengenezo na niwasihi watanzania kununua na kutumia aina hizi za pikipiki, kwanza bei zake ni rafiki na matumizi yake ni poa zaidi” alisema Afisa Operesheni Mkuu wa Sunbeam Auto Ltd Vinaykant Chaturvedi

Manara alisema, kwa kuwa bei za pikipiki hizi ipo hadi ya Sh milioni mbili na nusu na zinatumia vema mafuta.