January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Habari katika picha

Mwenyekiti wa ‘Alliance for Green Revolution in Africa’ (AGRA) na Waziri Mkuu mstaafu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn (aliyeketi watatu kutoka kushioto), na Mjumbe wa Bodi wa AGRA na Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete (aliyeketi wanne kutoka kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Ishmael Kasekwa (aliyeketi wa pili kutoka kulia), na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Derick Lugemala (aliyeketi kulia) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha JOYDONS (T) Ltd., kiwanda cha kuchakata mahindi na kusaga unga wa sembe Wilayani Bagamoyo. TADB imetoa mkopo wa kiasi cha sh. Bilioni 1.2 kwa kiwanda hicho kwa ajili ya kununua mashine za kisasa za kuchakata mahindi na kusaga unga wa sembe na ghala ya kisasa. Aliyeketi kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa AGRA, Vanessa Adams na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Sarah Msafiri.