January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gynah ashinda tuzo za LIPFF jijini Nairobi-Kenya

Na Mwandishi wetu TimesMajira Online

Mwandishi, muigizaji na mwanamitindo, ameibuka mshindi wa muigizaji bora kike kwenye tuzo za Lake International Pan African Film Festival(LIPFF) zilizofanyika usiku wa tarehe 6 November mwaka 2021, nchini Kenya na kuwabwaga waigizaji wengine kutoka, Afrika Kusini ,Cameroon, Morocco na Uganda

Tanzania ilikuwa pia kwenye kinyang’anyiro cha muigizaji bora kwa wanaume. Cojack Chilo aliyeigiza kwenye filamu ya “Nyara the kidnapping” aliteuliwa kushindana na nchi na Ghana, Uganda, Kenya, Afrika Kusini ambapo Rushabiro Raymond kutoka Uganda aliyeigiza filamu iitwayo “Stain” alishinda tuzo hiyo.


Pia kwenye kikundi cha filamu bora kipengele filamu ya “Nyara the kidnapping” kutoka Tanzania ilikuwa ikishindanishwa na Wateuliwa watatu kutoka Kenya na Uganda na tuzo ilienda kwa filamu ya Mission to rescue kutoka Kenya.

Iliyoambatanishwa ni orodha ya washindi wote wa LIPFF.

KUHUSU MULASI:
Mulasi ni neno la “kigogo” ambalo kwa Kiswahili linamaanisha “Rafiki”. Kabila la wagogo linapatikana mji mkuu au makao makuu ya Tanzania ambayo ni Dodoma. Mulasi (rafiki yangu) ni filamu kuhusu mwanamke aitwaye Sechelela ambaye an usongo wa mawazo ambapo anapitia kipindi kigumu kati yake na familia yake pia na kazi zake. Marafiki zake huwa pamoja naye wakati wote kumfariji wakiwa kwenye safari yao ya kutalii mji wa Dodoma.

Filamu imeongozwa na Honeymoon Aljabri mwenye tuzo za utengenezaji na uongozaji filamu, aliyezaliwa na kukulia Dodoma, Tanzania lakini makao yake ni Marekani. Honeymoon aliona bora kuigiza filamu hii mkoa alipozaliwa, Dodoma ili kukuuza utalii wake ambao bado haujachunguzwa na kuelezea filamu hii kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kukuza lugha na utamaduni wa nchi yake, Tanzania. Ameogelea mada ya kuhusu afya ya akili ili kuweza kuungana na hadhira ya kitanzania na ya kimataifa ambapo mada hii watu hupuuzia mara nyingi.

Regina Kihwele ni binti mwenye vipaji vingi aliyeigiza kama muigizaji mkuu Sechelela. Sechelela ni mwanamke jasiri anayebeba machungu mengi ambayo wanawake wengi wakitanzania kwenye ndoa zao huficha.

Tuzo hizi zimekuwa daraja la kukuza sekta ya filamu na utalii ya Tanzania kupitia waigizaji wadogo wadogo wa kike walioshinda tuzo hizo. Regina kama msanii na mtetezi wa afya ya akili anaamini kuwa filamu hii ni njia rahisi ya kueneza uelewa kwenye jumuiya ya Tanzania. Yeye anajiona kama mhamasishaji kwa waigizaji wengine wakike wenye matamanio na pia kuwa kama sehemu ya harakati kutamsaidia yeye kufanikiwa kwenye ndoto zake za kutengeneza filamu za aina ya elimu – burudani kutoka Tanzania.