January 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gulam, Bayi, Tandau wapeta TOC

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MGOMBEA pekee wa nafasi ya Urasi ndani ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 34 kati ya 35 zilizipogwa na wajumbe wa mkutano Mkuu uliofanyika jijini Dodoma ikiwa ni sawa na asilimia 97.14.

Gulam atasaidiwa na Makamu wake Henry Tandau ambaye ameshika nafasi hiyo baada ya kupata kura 30 sawa na asilimia 87.17 akimbwaga mpinzani wake Muharami Mchume aliyepata kura tatu sawa na asilimia 8.57.

Filbery Bayi ametetea nafasi yake ya Katibu Mkuu baada ya kuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo akipata kura 34 sawa na asilimia 97.14 huku Katibu mkuu Msaidizi Seleman Jabir naye akipata kura 34 kati ya 35 sawa na asilimia hizo 97.14.

Nafasi ya Mhazini Mkuu imechukuliwa na Charles Nyange aliyepata kura 31 na atasaidiwa na Juma Khamis Zaidi ambaye pia amepata kura 31.

Kwa upande wa wajumbe kwa Upande wa Tanzania Bara, walioshinda ni Noorlain G Shariff Sharif aliyepata kura 21 sawa na asilimia 60, Irene Mwasanga aliyepata kura 17 sawa na asilimia 48.58 na Qs Suma Mwaitenda ambaye pia alipata kura 17.

Wajumbe kwa upand e wa Zanzibar niMakame Ally Machano aliyepata kura 33 sawa na asilimia 94.28, Nasra Mohamed aliyepata kura 28 sawa na asilimia, Seleman Ame Khamis amepata kura 19 sawa na asilimia 54.28 huku Khalidi Lushaka akichukua nafasi ya mjumbe Kamisheni TOC.