November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Guatelama yakabiliwa na utapiamlo mkali

SAN MARCOS, Ripoti zinaitaja Guatemala kuwa ni taifa linaloshika nafasi ya 4 kwa kuwa na viwango vya juu vya utapiamlo duniani.

Kutokana na hali hiyo,mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani
(WFP), Shirika la Chakula Duniani (FAO) na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) changamoto hiyo inadhibitiwa kwa kuhakikisha mlo shuleni.

Aidha, kwa mujibu wa takwimu za Serikali na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) zaidi ya asilimia 50 ya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa kwa sababu ya kukosa lishe bora ambapo mji wa San Marcos umeathirika zaidi kwa utapiamlo.

Juhudi za WFP, FAO na IFAD zimewezesha wakulima ambao wanasambaza chakula chenye lishe bora katika shule mbalimbali mjini San Marco ili kupambana na utapiamlo shuleni kupitia mradi wa usambazaji chakula shuleni ulioanzishwa na mashirika hayo.