January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Guardiola: Man City itashinda rufaa yao

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola ana uhakika klabu hiyo kushinda rufaa yao waliopigwa marufuku kushiriki michuano ya Ulaya kwa muda a miaka miwili kutokana na kuvunja sheria za haki za fedha.

Man City walipeleka kesi yao katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo “CAS” na wanatarajia matokeo kuanzia Julai 13 mwaka huu.

Akizungumzia hilo Guardiola amesema, ana uhakika rufaa yao watashinda kwani klabu hiyo inahitaji kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya katika miaka hii.

“Tuko tayari, na nina uhakika tutaruhusiwa kucheza Ligi ya Mabingwa kwa sababu tunataka kuwa kwenye mashindano katika miaka hii,” amesema Guardiola.

City walipewa adhabu hiyo, na pia kupigwa faini ya euro milioni 30 (£25m) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya “UEFA” kwa “uvunjaji mkubwa” wa leseni za klabu na sheria za haki za Fedha.

Hata hivyo klabu hiyo, bado ipo kwenye Ligi ya Mabingwa iliyoahirishwa msimu huu na wanaongoza 2-1 hatua ya 16 bora dhidi ya Real Madrid baada ya mchezo wa kwanza huko Santiago Bernabeu.