Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
SHULE ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka 2023 / 2024 ikiwemo kujenga maabara, chumba cha compyuta, kuboresha na kuweka miundo mbinu yote kama madarasa, na vitendea kazi vyote kuwa bora kwa matumizi
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa shule ya sekondari Green Acres, Minani Kafugugu wakati wa mahafali ya 23 ya shule ya awali, msingi na kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Beach Salasala jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Dk. Nasib Mramba.
Amesema wamejipanga kuendelea kutoa taaluma bora na matokeo mazuri yenye tija kitaifa na kuwapa bima ya afya wanafunzi wote kidato cha kwanza hadi cha sita na kuongeza uhusiano wa shule na jamii yote majirani kiwilaya, mkoa na kitaifa
“Ubora wa elimu tuitoayo si katika taaluma tu, bali hata katika malezi na ustawi wa tabia, mwenendo wa afya kwa wanafunzi wetu hasa tukikumbuka kwamba tunaandaa taifa la kesho litakaloendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Ninaamini vijana wanaotoka Green Acres watakuwa mfano bora kwa wengine huko waendako,” amesema.
Amesema, ilikuwa na uhakika na ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi wake, shule imeweka utaratibu wa wahitimu wote kukaa bweni na kwamba utaratibu huo umesaidia kwa walimu kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja na kumsaidia kwa kadri ya mahitaji yake kitaaluma na kimalezi.
Amesema tangu waanzishe utaratibu huo wamekuwa wakipata matokeo mazuri sana kwa shule kufanya vizuri kwenye mitihani ya ndani ya mkoa na mitihani ya kitaifa kwa kushika nafasi za juu.
Aidha, amesema wameanzisha utaratibu wa kuabudu kwa itikadi zote yaani wakristo na waislamu ambapo kila mwanafunzi na mfanyakazi anapata nafasi ya kuabudu kwa imani yake na pia wameanzisha masomo ya dini yaani Elimu ya dini ya Kiislam (EDK na Biblia).
Amesema shule ya Green Acres imekuwa ikifanya vema kitaaluma kwa mitihani mingi ya kitaifa kidato cha nne mwaka 2021 wanafunzi waliosajiliwa walikuwa 26 wa kike 15 wa kiume 11 shule haikuwa na Daraja 0 na wote waliendelea na elimu ya kidato cha 5 na wengine vyuo vya kati, mnamo mwaka jana 2022, wanafunzi walifaulu kwa daraja la I, II na III tu na hapakuwa na Daraja la nne wako 0 wote waliendelea na masomo katika ngazi mbalimbali kama kujiunga na kidato cha tano, Vyuo vya Afya, Biashara na ualimu
Amesema licha ya ushindani mkubwa uliopo kwa shule za binafsi, shule hiyo imekuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika utoaji wa elimu bora, kutokana na msingi imara wa upendo na mshikamano uliojengwa na familia ya Green Acres pia mazingira bora na miundo mbinu iliyoboreshwa.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote