May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Na David John Timesmajira online Geita

KAMPUNI ya Nguvu Moja ( Security services limited ) inayoshughulikia sualapp0 ulinzi ni Moja ya Kampuni inayoshughulikia suala ulinzi sehemu mbali mbali imekua ikilinda afya ikijali afya ya wafanyakazi pamoja Mazingira wanayoishi pamoja na magonjwa.

Hayo yamebainishwa septemba 23 mwaka huu na Meneja wa Kampuni ya Nguvu Moja Services limited Caroline Mushi ambapo amesema kampuni hiyo imekua na tabia ya kuwapima afya wafanyakazi wake kabla ya kuingia kazini, na Mwaka mmoja akiwa kazini.

” Tunapoajiri wafanyakazi wetu, kitu cha kwanza sisi hatutaki mfanyakazi anayeugua ugua kazini, kwahiyo tunampima kabla hajaingia kazini, pia tutampima afya yake baada ya Mwaka mmoja akiwa kazini, vile vile ikitokea mfanyakazi akasema hawezi kuendelea na kazi na Nguvu Moja Security services au mkataba umekwisha, au amesema ameenda kusoma, pia tutampima afya yake.

“Tunampima kwa sababu gani tunataka tuhakikishe mfanyakazi tulivyompokea ana afya bora, anaweza kufanya kazi, na anapotoka ndani ya security services kule anapoelekea anakua na afya yake ile ile.”Amesema

Nakuongeza kuwa “kwasababu kumetokea magonjwa mbalimbali, kunatokea taadhari mbalimbali ambazo mtu hawezi kujua je hizi nimeipata nikiwa kazini au nilipata nikiwa napitapita katika miangaiko yangu ya kila siku” amesisitiza Meneja.

Amefafanua kitu kingine wanachoangalia kwa wafanyakazi wake ni Mazingira, Mazingira wanayofanyia kazi yawe safi, wanaangalia uvaaji wake, chakula chake anachotumia kila siku hili tunazingatia sana.

Pia amesema katika masuala ya kazi wamekua wakilinda sana afya ya wafanyakazi wao, hivyo wamejikita zaidi katika kuwapatia vifaa Bora vya eneo lao la kazi na kuwapatia elimu sahihi ya jinsi ya kutumia vifaa hivyo ikiwa ni sambamba na kuhakikisha wanavilinda vifaa hivyo ili vibaki katika hali nzuri.

Naye mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Nguvu Moja Security services limited Jacob Zacharia, ( Contract Meneja ) amesema cha kwanza wanahakikisha wanawapata Vijana ambao ni waadirifu, wazuri na waaminifu kutoka huko wanakotokea katika makazi ya kawaida.

” Kabla ya kuwaajiri wanahakikisha wanawafanyia vipimo vya uhakika baada ya kujilidhisha kwa wale waliotuma maombi baada ya kujilidhisha nao wanakwenda katika hatua ya pili ni kuwaajiri Vijana wenye sifa waliopitia JKT na waliopitia mgambo” amesema Zacharia.

” Lakini pia kwakua hii ni kampumi ya kizalendo ya kitanzania haibagui watu wote, tunaajiri hata watu ambao ni raia wa kawaida ni wale ambao wanataluma ya kutosha, waaminifu ambao pia wanaweza kusaidia Kampuni hii kuweza kusonga mbele.

Amefafanua kuwa Kampuni hiyo inaanza kuajiri kuanzia darasa la sana, kidato cha nne, kidato cha sita, diploma ,digrii na kuendelea kulingana na uhitaji na utaalam unaotakiwa.

Amesema Kampuni ya Nguvu Moja Security services haina ubaguzi kwenye kuajiri, kila mwenye sifa na kila ambaye anastahili basi atapata ajira katika Kampuni hii ya Nguvu Moja.

Hata hivyo Operation Meneja,Desideri Stevin Amesema Kampuni hiyo imejikita kwenye maeneo la migodi ambayo wanatoa aina tofauti tofauti za huduma za kiaskari lakini pia wanawakaribishan Taasisi ,mashirika mengine Ikiwa pamoja na mtu mmoja mmoja mwenye kuhitaji huduma za kiulinnzi basi wako tayari kufanya nao kazi na gharama Zao ni za kawaida .