ROME, Italia
RAIS wa Shirikisho la Soka Nchini Italia (FIGC), Gabriele Gravina ameitaka Juventus kutokubali kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Italia Serie A msimu huu, iwapo ligi hiyo itashindwa kumalizika kutokana na janga la virusi vya Corona.
Kwa sasa Juventus chini ya kocha wake, Maurizio Sarri kabla ya Ligi hiyo Kusimama ndio vinara wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 63 moja zaidi ya Lazio baada ya kucheza mechi 26 msimu huu.
Barani Ulaya, Italia ndio Nchi yenye Wagonjwa wengi na Vifo ambapo kwa sasa imeripotiwa kufikia vifo 15,362 huku Walioambukizwa Virusi hivyo ni watu 124,632.
Mapema ilitangazwa kuwa ligi hiyo ingeendelea Aprili 12, mwaka huu, lakini hadi sasa hakuna tarehe maalumu ya ligi hiyo kurejea.
Gravina alisema itakuwa sio haki kusitisha msimu, hivyo wanafikiria kuendelea na ligi kuanzia mwezi Mei au mwanzoni mwa mwezi Juni na imalizike Julai, wakati huo huo kumekuwa na mazungumzo ya kuifanya ligi hiyo kucheza Kati ya Agosti na Septemba.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM