January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gnako Warawara atangaza rasmi EP yake

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva kutoka kundi la Weusi G Nako Warawara, ametangaza rasmi jina la EP yake ambayo amekuwa katika maandalizi yake kwa muda mrefu.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram, EP hiyo ya ‘Kitimoto’ ambayo itakuwa na Nyimbo kama Sita na zote zitakuwa ni Club Banger.

”Sijui nitoe Wimbo Mpya anyway EP yangu inaitwa ‘Kitimoto’, kWA furaha tu dah mngefunga leo manyoya, Kitimoto EP on the way,” ameandika Gnako Warawara.