December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gigy Money: Ndoto zangu zimetimia kufanya kazi na JB

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Video Queens machachari hapa nchini, Gift Stanford maarufu kama ‘Gigy Money’ amesema ndoto zake zimetimia kufanya kazi na msanii wa bongo movie Jocob Steven (JB).

Akizungumzia hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram huku akishare picha yeye yeye na JB, Gigy Money amesema alikuwa akimtazama JB tokea alipokuwa shule, hivyo amefarijika sana kufanya kazi na msanii huyo.

“Tutoe kipaji ulicho kiona kwangu, wewe ni mtu ambae tangu nipo shule nakutazama, nakuona Na nakuangalia lakini kufanya kazi kuwa ata karibu yako kwangu ni moja ya ndoto zangu, kwani najua nimejitafuta Sana ila nimejipata, nilikua Na ndoto yakuifikisha hii tasnia yetu mbali kwa pamoja.

“Napenda Movie Sana Na nusu ya maisha yangu ni Tamthilia. Nampenda sana JB sana, Asante sana kwa kunipa nafasi hakika sitakuangusha,” amesema Gigy Money.