December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gigy Money ampa makavu Diva

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva mwenye vituko vingi hapa nchini, Gift Stanford maarufu kama ‘Gigy Money’amempa makavu mtangazaji wa Wasafi FM Divatheebawse na kumtaka kuacha mara moja kulitaja jina anapokuwa kwenye kipindi.

Akitoa makavu hayo, Gigy Money amesema,anamuheshimu sana mtangazaji huyo, hivyo hataki kusikia jina lake akilitaja ovyo kwani wanampa shida mtoto wake kila kukicha kusikia jina la mama yake likitajwa kwenye vyombo vya habari.

“Hivi mshajiuliza kwanini kipofu hana Macho lakini anaona Kinyaaa?. Maisha ya instagram pia yanachosha kwani Dada Diva mtu akija kwenye kipindi chako huwezi kumuuliza hata kama anajua umri wako.

“Sipendi unavyofanya, jina langu kama mimi nagombana na hao madem, yani sio fresh kama inakupa airtime kwasababu ba mtoto wangu pia anakipindi cha usiku izo ni biashara zenu Dada diva, acha kuwauliza watu kuhusu mimi sipendi.

“‘I GO THROUGH MY HARD TIMES ALONE SO LEAVE ME ALONE’, nakueshim sana na nina maisha yakutegemewa, huu muda mnaotaja jina langu ovyo mnampa mwanangu shida yakuelewa kila siku mama yake midomoni, sitaki nyie ni wakubwa sana kiumri acheni Drama za kizamani.

“Usipereke kipindi kama jumba la michambo nakudharilishana, sitaki kama kosa kutokuja kwenye kipindi chako siku ile basi sitaki kugombana, mimi mkubwa sasa hivi sipendi Dada angu sio vizuri kila nikiamka nakuta wewe na baadhi ya watu mnaniongelea afu sio vizuri, vibaya kwani hapa watu wanataka kuniongelea hawana mema niliyo wahi kuwafanyia. Eti ‘this is my interview’, sitaki nyie wamama wakubwa sasa japo hamjazaa,” amesema Gigy Money.