YAIPUA WIMBO WA NI SIKU YETU KWA AJILI YA HARUSI
Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
KWAYA ya Gethsemane Group Kinondoni(GGK) SDA ya jijini Dar es Salaam imeipua wimbo wake mpya maalumu kwa ajili ya Harusi ujulikanao kama Ni Siku Yetu.
Wimbo huo umetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita tayari upo kwenye mtandao wa YouTube umepokelewa vizuri na mashabiki pamoja na wapenzi wa muziki wa Injili nchini.
Akizungumza kuhusu wimbo huo wa harusi unaojulikana kama Ni Siku Yetu Kiongozi wa Kwaya ya Gethsemane ambaye pia ni Mwenyekiti Samora Sadick amesema lengo la wimbo huo ni kuwabariki maharusi na wimbo unaomtukuza Mungu siku ya harusi yao.
Amesema Wimbo umerekodiwa Kwenye studio maarufu ya Katumbo Music ya jijini Dar es salaam.Video ya wimbo huo imefanywa na muongozaji mashuhuri nchini Director Joowzey.
“Mikakati ya kundi baada ya wimbo huu ni kuzindua album mpya inayotarajiwa kutoka mwaka huu 2025. Kwaya ya Gethsemane inatoa mwito kwa waimbaji wengine kuendelea kutoa nyimbo za kumtukuza Mungu na kutoa mafundisho mbalimbali Kwenye jamii.
“Kwaya ya Gethsemane group Kinondoni (GGK) SDA inaendelea kujivunia kuwa kwaya iliyojikita katika huduma zaidi ikiwa imepata nafasi ya kutoa huduma ya uimbaji kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo ndani na nje ya nchi. Mwaka 2024 GGK ilipata mialiko miwili ya kuhudumu katika mikutano mikubwa ya injili ya Makambi jijini Nairobi nchini Kenya,”amesema
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio