Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOnline,Dar
WAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa Bwana Wastahili.
Video ya wimbo huo imeachiwa Machi 18,2024 saa mbili usiku na umerekodiwa katika Studio ya Flying Wave Studio na kuongozwa na Director maarufu ajulikanae kama Director Joowzey.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya video hiyo kuachiwa hewani (kuzinduliwa) Mwenyekiti wa Gethsemane Group Kinondoni GGK Geoffrey Joseph alisema ni furaha kwao kuja na video ya wimbo huo ambayo imebeba ujumbe wa kumuabudu na kumtukuza Mungu.
“Ujumbe mkubwa kwenye wimbo huu ni kwamba Mungu pekee ndiye anastahili kuabudiwa na yeye ndiye anatosha kwa kila kitu hasa kipindi hiki ambacho baadhi ya madhehebu wapo Kwenye mfungo, tunaamini wimbo huu ni ibada na utawasogeza karibu zaidi na Mungu,”amesema Joseph
Aidha ametoa neno kwa wasikilizaji na Watazamaji wa video ya wimbo huo kutambua hakuna yoyote anayestahili kuabudiwa zaidi ya Mungu pekee.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA