April 24, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Fyandomo amnadi Dkt.Tulia kwa wananchi Mwasanga, amfananisha na dhahabu

Na Esther Macha,TimesMajiraOnline,Mbeya

MBUNGE mteule wa Vitimaalum Chama Cha Mapinduzi(CCM) kupitia mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo amesema kuwa Dkt.Tulia Ackson anastahili ushindi wa heshima ili aweze kushughulikia changamoto walizonazo kata ya Mwasanga ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya msingi na miundo mbinu ya barabara.

Akizungumza wakati wa kumnadi Dkt.Tulia katika kata ya Mwasanga, Fyandomo amesema wananchi wa Uyole wamepata bahati kubwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Mbeya Mjini, kwani sasa wana kiongozi mwenye heshima kubwa duniani kama Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani.

“Nilidhani dhahabu hupatikana Chunya pekee, lakini sasa wananchi wa Uyole wamebahatika kupata dhahabu yao kupitia mgombea ubunge wa jimbo hili Dkt. Tulia Ackson.

“Ndugu zangu wa Mwasanga,nimekuja kwa unyenyekevu mkubwa kuomba kura za mafiga matatu yani Rais, Mbunge na Diwani. Kazi zao  zinajieleza twende sote tukapige kura kwa pamoja ili tuweze kuletewa maendeleo “amesema.

Fyandomo ameongeza kuwa wananchi wa Uyole wanapaswa kumpa kura za ushindi Dkt. Tulia ifikapo Oktoba 29, ili aendelee kuibuka kidedea kwenye uchaguzi mkuu.

“Dkt.Tulia na Rais Samia wanazungumza lugha moja. Tukimchagua yeye atuletee maendeleo yatakwenda kasi.Nawaomba tusikosee tarehe hiyo muhimu,” alisisitiza.