Na Penina Malundo,Timesmajira
WITO umetolewa kwa Watanzania ambao wanasifa ya Udereva wa Mabasi Makubwa(Mwendokasi) kuchangamkia fursa za ajira nchini Qatar ambazo zimetolewa na Serikali ya nchi hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kuhitaji takribani madereva 1150.
Miongoni mwa vigezo vinavyohitajika katika kazi hiyo ni pamoja na umri wa dereva kuwa kati ya miaka 25 hadi 50,Leseni ya Udereva ya alama ya Class C1,C2 na E,hati ya kusafiria na kuwa na Afya Bora.
Akitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Asasi za Ajira nchini chini ya Mwamvuli wa Chama cha Mawakala wa Ajira nchini(TRAA) na Mkurugenzi wa Kampuni inayojihusisha na masuala ya usafirishaji Al Maha Travel,Abdallah Mohamed wakati akitangaza fursa hiyo kwa waandishi wa habari.Alisema usahili wa zoezi hilo unatarajia kufanyika Aprili 4 mwaka huu na kutarajia kuwakusanya takribani madereva 3000 ili kupata idadi hiyo wanayohitaka kwaajili ya kuwasafirisha na kuwapeleka nchini Qatar.
”Kampuni iliyopewa dhamana ya kusimamia zoezi hili ni sisi Kampuni ya Al Maha Travel kwa upande wa huku Bara na kwa upande wa Zanzibar ni kampuni ya Kemmy ambapo kwa Tanzania Bara wanatakiwa kupatikana Madereva 900 na Zanzibar 250.
”Tunaomba Watanzania mjitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hii ambayo haina gharama yoyote na wala hatutozi kitu chochote,namna ya watu kujisajili wanaweza kutumia Kampuni mbalimbali za ajira nchini au kufika katika Ofisi za Kampuni ya Al Maha Travel hapa Salamanda na kujisajili,”Amesema.
Aidha amesema Usahili rasmi wa fursa hiyo kwa upande wa Tanzania Bara unatarajia kufanyika ndani ya siku tatu kuanzia Aprili 6 hadi 8 mwaka huu na kuchukua takribani watu 300 kwa siku hadi kukamilisha idadi ya watu wanaohitaji huku kwa Zanzibar usahili unatarajia kufanyika kwa siku moja.
”Hizi kazi ni za bure,hazilipiwi senti tano hizi juhudi sio za kwetu sisi binafsi zimefanywa na Serikali kwa ujumla ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia balozi wake nchini Qatar,”amesisitiza Mohamed
Amesema mishahara ni mizuri zaidi ya Dolla 700 wanalipa ambayo ni fedha ya kurudi nayo nyumbania ambapo kwa hela ya Tanzania ni sawa na Milioni 1.8 huku ukihudumiwa kila kitu bure ikiwemo Makazi,Usafiri na Matibabu

More Stories
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama
Kihongosi amtaka mkandarasi kuwalipa vibarua stahiki zao
DC Mbozi afuturisha wananchi, asisitiza mshikamano na Umoja.