July 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

FMJ yajivunia mazingira mazuri ya uwekezaji

Picha zote Inaonesha bifhaa mbalimbali za ujenzi zinazopatikana FMJ Hardware

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online

KAMPUNI ya vifaa vya ujenzi FMJ hardware imeipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwenye sekta ya uwekezaji na biashara na hivyo kuwawezesha hata wazawa kufanya biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea banda la serous kwenye maonyesho ya 48 ya Kmataifa ya Biashara 77 Jijini Dar es Salaam Afisa masoko,Jacqueline Yanga amesema wao kama wauzaji na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi wamekuja kuonyesha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu .

Amesema serikali ya awamu ya sita imejipambanua kwa sababu imewapa wawekezaji hususan wazawa wigo mpana kwenye sekta ya uuzaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo za ujenzi .

Ameongeza kuwa FMJ hardware ni kampuni ya kizawa na ipo kwa ajili ya Watanzania wote na hata kwa nchi jirani kwa maana ya Afrika mashariki kwani inasambaza vifaa hivyo hadi hizo nchi za jirani.

Ameongeza wapo tayari kuwahudumia wananchi kipindi hiki cha 77 na hata baada ya 77 kwani ofisi zao zipo jijini Dar es laam Buguruni kisiwani.

“Ndugu wananchi wa Dar es laam na viunga vyake mnakaribishwa kwenye banda la serous kuja kujionea bidhaa bora kutoka FMJ HARDWARE”, amesema Jacqueline

Ameongeza kuwa kampuni hiyo inasambaza vya ujenzi vya aina zote.