Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
JUHUDI za Rais Samia za kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya The Royal Tour zimeanza kuzaa matunda kwa wageni wengi kutoka nje ya ncui kutua katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) huku ikielezwa kumekuwa na ongezeko la abiria kutoka 347,757 mwaka 2020/21 hadi kufikia abiria 654,159 mwaka 2021/22 ni sawa na ongezeko la asilimia 88.
Akizungumza jijini Dodoma na waandishi wa habari Mtendaji Mkuu wa kampuni ya KADCO ambayo ni kampuni ya Kiserikali ya uendelezaji na uendeshaji wa kiwanja Cha ndege Cha Kilimanjaro (KIA) Christine Mwakatobe amesema, hayo ni miongoni mwa mafanikio katika utekelezaji wa shughuli za KADCO.
Aidha ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana ni kupitia shirika jipya la ndege la Eurowings Discover(part of Lufthansa Group) iliyoanza safari zake kutoka Frankfurt,Ujerumani kwenda KIA kuanzia mwezi Juni mwaka huu,shirika hilo linachangia kuongeza idadi ya abiria na mizigo.
“Kuendelea kuwa na mashirika mbalimbali ya ndege za kukodi(charter flights)ambayo yameendelea kutumia KIA kwa kuleta makundi maalumu ya watalii kutoka sehemu mbalimbili duniani,
Kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya Nchi kuwekeza KIA katika maeneo tofauti ikiwemo hotel za kisasa,maeneo ya biashara mchanganyiko(business Complex)na jengo la wageni mashuhuri(CIP lounge facility),”Ameeleza.
Kwa mujibu wa Mwakatobe hali ya uendeshaji uliendelea kuimarika hadi mwaka wa fedha 2020/21 ambapo Dunia ilikumbwa na janga la Uviko 19 lililoathiri sekta nyingi za kiuchumi Duniani ikiwa ni pamoja na sekta ya usafiri wa anga.
“Katika kipindi hicho shughuli za uendeshaji KIA zilishuka kwa kiasi kikubwa kutokana na nchi nyingi kufunga anga ikiwa ni njia moja wapo ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo,hii ilipelekea idadi ya abiria kushuka kwa kiwango kikubwa kutoka laki 794,337 mwaka 2019/20 hadi kufikia abiria laki 347,757 katika kipindi Cha mwaka 2020/21 ikiwa ni punguzo la abiria kwa asilimia 56.”amesema na kuongeza kuwa
“Kupunguza kwa shughuli za uendeshaji KIA kuliathiri mapato,ikizingatiwa kwa chanzo kikuu Cha mapato ya KADCO ni tozo zinazotokana na abiria wanaopita KIA pamoja na kutua na kuruka kwa ndege kiwanjani,hali hii ilipelekea menejimenti ya KADCO kuchukua hatua ya kubana matumizi na kusimamisha kwa muda baadhi ya shughuli za maendeleo ili iweze kupita Katika kipindi hiki kigumu ikiwa inaendelea kujiendesha,
Hata hivyo nikiri kuwa kipindi hiki tukiendelea kutoa huduma kwa kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa wakati wa janga la Uviko-19 na kutambuliwa kama moja ya viwanja kilichofanya vizuri zaidi katika kipindi hicho kwa kuzingatia maelekezo ya kujikinga yaliyokuwa yanatolewa kupitia Wizara yetu ya Afya,”amefafanua.
More Stories
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia