

PPRA YATOA MAAGIZO NANE KWA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA.
Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) Denis Simba ,ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanzisha haraka michakato ya ununuzi inayohusu fedha za Mfuko wa Jimbo ndani ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST).
Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023,imeanza kutumika Juni 2024,ikitajwa kuwa na mafanikio mengi ikiwemo kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Akifungua Mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa NeST jijini Dodoma kwa Wakurugenzi, Wataalamu wa TEHAMA na Maofisa Ununuzi ngazi za Mikoa na Halmashauri Simba amesema , ni lazima wahakikishe mchakato huo unaanishwa kwenye maeneo ambayo fedha zake zipo na hawajaanzisha ndani ya mfumo wa NeST.
Simba amesema Moja ya changamoto zinazoikabili Serikali za Mitaa ni pamoja na makisio ya bajeti yasiyo ya una hivyo kusababisha washindi wa zabuni kutopatikana.
“Katika kuhakikisha changamoto hiyo inatatulika, PPRA itashirikiana nanyi Ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi .”amesema Simba
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ,PPRA ipo mbioni kukamilisha uimarishaji wa mfumo na kuwa suluhisho kwa kitumia TEHAMA ili kuwabaini wale wajanja wanaodhani mfumo huo hauna macho.
More Stories
Dkt.Biteko awataka wanawake kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia
Biteko: Afrika tunayapa kipaumbele matumizi Nishati Safi kukabiliana mabadiliko ya Tabia nchi
Mhandisi Mahundi:NBC yaunga mkono Serikali kidijitali