March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Fani ya nyama inavyoweza kuwakomboa wananchi kiuchumi

Na Joyce Kasiki,Dodoma

MAMLAKA ya Mafunzo na Elimu ya Ufundi Nchini inawakaribisha vijana na wananchi kwa ujumla kujifunza fani mbalimbali ikiwemo fani ya nyama ambayo inapatikana katika chuo Cha VETA Dodoma.

Akizungumza Agosti Mosi ,Mwaka huu katika maonyesho ya wakulima na wafugaji Nane Nane yanayoendelea jijini Dodoma,Mwalimu wa VETA Dodoma Veronicah Assewe amesema,katika chuo hicho wanafundisha fani ya nyama ambayo humwezesha muhitimu kujiajiri kwa kufungua duka lake la nyama huku akiwa na ujuzi wa kutosha kuhusu masuala ya nyama.

Amesema,mwanafunzi anafundishwa kutengeneza bidhaa mbalimbali za nyama kama vile soursage,kuandaa supu,na kuhifadhi vichwa vya mfugo husika ili kuepusha upotevu wa mavuno ya mazao ya mifugo.

“VETA tunamfundisha mwanafunzi vitu vingi sana kwenye fani ya nyama ikiwemo kukata mikato tofauti tofauti ya nyama ,lakini pia mwanafunzi akihitimu VETA anakuwa ameiva na anakuwa na uwezo wa kuahiriwa na wenye maduka ya nyama na hata kufungua lake na akaweza kufanya kazi vizuri.”amesema Assewe

Vile vile amesema wanafundisha kukata nyama kwa kutumia mashine na siyo magogonambayo watu wengi Bado wanatumia kitu ambacho ni hatarinkwa Afya za walaji

Amewaasa wale wote wanahitaji kujifunza fani ya nyama ikiwa ni pamoja na kuchinja mifugo,kufika chuo Cha VETA Dodoma Ili waweze kupata ujuzi utakaowasaidia kujikwamua kiuchumi.