February 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Fainali Khimji cup kufanyika Februari 7,2025

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

FAINALI ya mashindano ya mpira wa miguu kugombea kombe la Kimji (Kimji super cup) yanatarajia kufanyika Februari 7,mwaka huu katika uwanja wa Garden Ilala.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Ilala, Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Kimji ,amesema mashindano hayo ya mpira miguu, yalioanza hivi karibuni ambayo yameandaliwa na ofisi yake kwa kushirikiana na Chama cha Mpira Miguu (IDFA),Wilaya ya Ilala,yatafanyika Ijumaa ya Februari 7,2025 ambapo burudani mbalimbali zitakuwepo .

Amesema dhumuni la michezo hiyo ni kukuza vipaji kwa timu za Ilala na kuinua vipaji kwa vijana kwani michezo ni afya, michezo ni ajira.

“Fainali hii ya Khimji Super Cup,itashirikisha timu ya Kasuru FC na Searose FC zote kutoka Ilala, nawaomba wananchi wa Kata ya Ilala na pembezoni,ujitokeze kwa wingi,awali katika ufunguzi timu mbalimbali zilishiriki kuanzia hatua ya mtoano,robo fainali mpaka nusu fainali, “amesema Khimji.

Sanjari na hayo amesema katika fainali hiyo iliyopewa jina Khimji Ilala fun day 2025 FUN DAY 2025,mgeni rasmi anatarajiwa kuwacMwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mkoa wa Dar- es -Salaam Abbas Mtemvu na wageni maalum.