
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Exim Tanzania imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 kwa kusisitiza dhamira yake ya kuendelea kutoa huduma bora, zenye mwitikio na zinazomweka mteja mbele, kupitia kaulimbiu ya mwaka huu, “The Extra Mile.”
Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo, wafanyakazi wa Benki ya Exim walishiriki katika matembezi ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, yakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Jaffari Matundu, ikiwa ni ishara ya wazi ya dhamira ya Benki ya kumweka mteja katika kiini cha kila jambo linalofanywa.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Matundu amesema kwenda “The Extra Mile” akimaanisha kumweka mteja kwanza na kuhakikisha kuwa kila mwingiliano na mteja unaongeza thamani kwake. Alisisitiza kuwa huduma bora kwa wateja ni jukumu la pamoja ndani ya Benki, ambapo kila mfanyakazi ana nafasi ya kuhakikisha huduma za kibenki zinakuwa rahisi, zenye urahisi zaidi na zenye mwitikio kwa mahitaji ya wateja.



More Stories
Tanzania yashiriki CPHI Milan 2026
Waandishi wa Oman watembelea UDSM, TBC wapongeza JOWUTA.
Elimu ya Udhibiti yawafikia wenye ulemavu Tabora