Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), George Mhina,ameeleza kuwa mamlaka hiyo kila mwaka inatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kurudisha kwa jamii ambapo mwaka huu imetoa madawati 25 yenye thamani ya takribani milioni kwa shule ya msingi Mandela iliopo mtaa wa Kikwete Kata ya Igoma jijini Mwanza.
Mhina ameeleza hayo wakati akizungumza na Timesmajira Online ofisini kwake jijini Mwanza hivi karibuni ambapo ameeleza kuwa madawati hayo waliyakabidhi Machi 25,2024 ikiwa ni mchango wa EWURA kama sehemu ya kurudisha kwa jamii.
Ameeleza kuwa sababu ya kutoa madawati hayo katika shule hiyo ni kutokana na uhitaji uliopo kwani watoto walikuwa wanakaa chini hivyo walizungumza na uongozi wa Kata ya Igoma kupitia Diwani wa Kata hiyo.
“Tunafanya hivyo kila mwaka pale kadri tunavyokuwa na fedha na tumeamua kuwekeza kwenye shule za msingi kama wadau wa elimu ikiwa ni semehu moja wapo ya kuchangia maendeleo ya elimu kwa mwaka huu katika kata hiyo,”.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili