Na Zena Mohamed,TimesmajiraOnline,Dodoma.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA),imetoa bei kikomo za mafuta ya petroli nchini zinazoanza kutumika kuanzia kesho huku ikisema Serikali itapoteza bilioni 30 kwa mwezi kutokana na hatua iliyochukua ya kuhairisha tozo ya shilingi 100 kwa lita kwenye bidhaa za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo kuhusu bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo amesema bei za rejareja na jumla za mafuta ya petroli, Dizeli na mafuta ya Taa yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar Es Salaam zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la Februari 2 mwaka huu.
Ambapo amesema kwa mwezi huu bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka kwa shilingi 60 kwa lita sawa na asilimia 2.42 na shilingi 65 kwa lita sawa na asilimia 2.77 mtaliwa huku bei ya mafuta ya taa ikipungua kwa shilingi 83 kwa lita sawa na asilimia 3.63.
Ameeleza kuwa bei hizo zingeweza kuwa juu zaidi kama serikali isingechukua hatua ya kuhairisha tozo ya shilingi 100 kwa lita kwenye bidhaa za mafuta ya petroli,Dizeli na mafuta ya Taa.
“Mabadiliko haya ya bei yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika soko la Dunia,gharama za usafirishaji(BPS Premium) na thamani ya shilingi ukilinganisha na dola ya kimarekani,”amesema.
Poa amesema bei za jumla za petroli na dizeli zimeongezeka ikilinganishwa na mwezi uliopita ambapo petroli imeongezeka kwa shilingi 59.65 kwa lita sawa na asilimia 2.54,dizeli 64.45 kwa lita sawa na asilimia 2.92 mtawaliwa huku bei ya jumla ya mafuta ya taa ikishuka kwa shilingi 82.67 kwa lita sawa na asilimia 3.82.
Akizungumzia Mikoa ya Kaskazini ambayo ni Tanga,Arusha na Manyara amesema bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka ikilinganishwa na bei za mwezi uliopita ambapo petroli imeongezeka kwa shilingi 165 kwa lita sawa na asilimia 6.88 na dizeli shilingi 207 kwa lita sawa na asilimia 9.09.
Kwa bei za jumla za petroli na dizeli pia amesema zimeongezeka petroli kwa sshilingi 164.76 kwa lita sawa na asilimia 7.26 na dizeli kwa shilingi 206.62 kwa lita sawa na asilimia 9.62.
Kwa Mikoa ya Kusini ambayo ni Mtwara,Lindi na Ruvuma bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka ikilinganishwa na mwezi uliopita ambapo petroli imeongezeka kwa shilingi 43 kwa lita sawa na asilimia 1.70 na dizeli kwa shilingi 105 kwa lita sawa na asilimia 4.35,mtawaliwa na bei za jumla kwa petroli imeongezeka kwa shilingi 43.27 kwa lita sawa na asilimia 1.80 na dizeli kwa shilingi 105.57 kwa lita sawa na asilimia 4.60 ,mtawalia.
“Kwakua hakuna matanki ya kuhifadhia mafuta ya taa Mtwara waendeshaji wa vitu vya mafuta kwenye mikoa ya kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya Taa Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya Taa kupitia bandari ya Dar Es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika,”amesema Kaguo.
More Stories
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa