December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

EWURA yatangaza bei mpya za mafuta ya petroli

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa chini zitakazotumika kuanzia Leo Agosti 02, 2023 ambapo kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dares Salaam petrol itakuwa ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 a mafuta ya taa 2668.

Taarifa kutoka EWURA imesema mabadiliko ya bei hizo yanatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani.